Sehemu ya Pili – Ujasiriamali | Sifa, Mtazamo na Matendo ya Mjasiriamali

DSC04927

Sifa, Mtazamo na Matendo ya Mjasiriamali

Anayo nia na ari ya jambo aliloamua kulifanya.

 • Ana uwezo wa kutoa uamuzi mapema hata kama ni mgumu.
 • Yuko tayari na hujitolea yeye binafsi.
 • Hufanya kazi yake kwa nidhamu ya juu.
 • Hakati tamaa.
 • Ana uwezo wa kutatua matatizo

Hupenda kutumia fursa inayojitokeza kikamilifu.

 • Anatambua mahitaji ya wateja wake kwa uhakika.
 • Anajua na kufuata mwelekeo wa soko.
 • Anapenda kufanya kitu ambacho kinaonekana mbele ya jamii.
 • Hafanyi mambo kwa pupa.

Anao uwezo na kipaji cha kuwasiliana, kuongoza pia kushawishi na daima yuko mbele kwa kila analotenda.

 • Anapenda kushirikiana
 • Anapenda kuwahamasisha wengine
 • Anaheshimika na anaaminika.
 • Mpenda haki.
 • Hupenda kujifunza na kufundisha wengine.
 • Hukubali wengine kumkosoa
 • Hana ubinafsi.

Mvumilivu, yupo tayari kuchukua uamuzi ambao unaweza kuhatarisha biashara yake na kwake binafsi.

 • Mpenda kujitosa – liwalo na liwe.
 • Hushirikisha wengine katika matatizo ya biashara.
 • Ana uwezo wa kufanya biashara kwenye mazingira yaliyoeleweka.
 • Huvumilia hata penye mambo ambayo hana uhakika kama yatafanikiwa.
 • Hujitia moyo hata kama mambo yakienda vibaya.
 • Anayo nia na ari ya kutenda.

Ana ari na msukumo mkubwa wa kufanikiwa katika shughuli zake.

 • Anajua uwezo na upungufu wake.
 • Anapenda ushindani wa maendeleo
 • Anaweka malengo ya juu lakini anayoweza kutekeleza.
 • Anapenda kuweka malengo na kufanya kila liwezekanalo ili kufanikisha azma yake.
 • Hapendi kulaumu pale anaposhindwa kutimiza malengo yake.
 • Hapendi malumbano, bali hutafuta mbinu za kupambana na vikwazo.
 • Ni mpenda watu na daima mwenye furaha.

Mtundu, Mbunifu na Mpenda kujitegemea

 • Ni mbunifu katika kupambana na kutatua matatizo.
 • Ana uwezo wa kujifunza kitu kwa haraka.
 • Haogopi kushindwa.
 • Ana uwezo wa kuzoa mawazo pia mambo mapya kwa haraka
 • Ana uwezo wa uchambuzi wa hakika kwa manufaa ya biashara yake.
 • Mpenda mabadiliko.

Kujiwekea malengo ya muda mfupi na mrefu.

 • Hupenda kufanya kazi zake kwa mpangilio maalumu.
 • Hutazama mbele.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.