Utekelezaji wa wazo la biashara
Ili wazo la biashara liweze kutekelezwa, yako mambo makuu matano ya kufanya:
Mpangilio wa wazo la biashara kwa mfano
- Aina / hali ya biashara unayoiwaza
- Nani atakayemiliki biashara hiyo – familia, ubia, kikundi n.k.
- Aina ya leseni inayohitajika – grosari, vileo, mgahawa, duka n.k.
Bainisha soko kwa kutilia maanani mambo yafuatayo
- Aina ya bidhaa/huduma utakayotoa na kwa wateja gani?
- Mbinu zitakazotumika ili uweze kuwa tofauti na washindani wako ili biashara ivutie wateja.
- Njia bora zaidi ya usambazaji na uuzaji.
- Eneo bora na nafuu kwa biashara yako.
- Namna ya kutangaza biashara yako.
Fikiria namna ya kupanga na kuendesha biashara yako
- Utahitaji vifaa vipi na wauzaji wake ni nani.
- Ni huduma gani na ukarabati gani wa vifaa unahitajika.
- Malighafi utaipata kutoka wapi.
- Namna ya kuchagua na jinsi ya kuwamotisha wafanyakazi ulionao.
- Fikiria namna ya kupanga uzalishaji na uuzaji wa bidhaa zako.
Uchambuzi wa fedha
- Chambua gharama za uzalishaji.
- Upangaji wa bei.
- Fanya makisio ya faida na hasara.
- Fanya makisio ya kitega uchumi na mtaji wa kazi.
Mipango
- Weka mipango na hatua za kuchukua ili kuanza utekelezaji kidogo kidogo.
- Pangilia fedha iliyopo.
- Panga hatua za kutekeleza wazo la biashara.
- Pangilia kwa makini huduma inayohitajika na mahali inapopatikana.
- Bainisha njia mbalimbali za kupata fedha kwa njia ya vitega uchumi.