Sehemu ya Tano – Ujasiriamali | Wazo la Biashara

DSC04983

Wazo la Biashara

Maana ya wazo la biashara

Kabla mtu hajaanza biashara, huwa anaanza kupata wazo la nifanye nini? Mawazo haya hupitia hatua kuu mbili:

Hatu ya kwanza

Mawazo mbalimbali humiminika kichwani kwa mfano: sijui jinsi ya kuanzisha duka, sijui kuuza nyama, sijui kufanya usafi.

Mawazo ya namna hii huitwa mawazo ghafi kwani hayajachujwa. Pamoja na hayo, mawazo haya hayajafanyiwa uchunguzi wa awali kama yatatekelezeka. Kama utaanzisha biashara katika hatua hii, uwezekano wa kuanguka ni mkubwa.

Hatua ya pili

Wazo ghafi hutathiminiwa, na kama litaonekana kuwa linaweza kutekelezeka kuwa biashara kamili huitwa wazo muafaka. Pamoja na kuwa na wazo muafaka, mafanikio ya biashara hutegemea uwezo wa mtekelezaji au mtafutaji.

Kubuni wazo la biashara ni muhimu kwa mtafutaji kwa sababu zifuatazo:

  • Ni hatua ya kwanza kabla ya kuanza biashara yoyote ile.
  • Ni muhimu ili kufanya biashara ifanikiwe.
  • Mara kwa mara wateja hubadilika na kupendelea vitu vingine ambavyo ni tofauti na vile vilivyopo.
  • Mabadiliko ya tekinolojia ni endelevu.
  • Athari zinazoikabili biashara yako.
  • Ni muhimu kwa mafanikio ya biashara yako.
  • Kutokana na mianya na nyanja za biashara pindi zinapojitokeza.
  • Hali duni ya maisha.
  • Ongezeko la mahitaji ya watu.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.