
Gundua wateja wanataka nini
- Ufanisi
- Unafuu wa bei
- Ukaribu
- Starehe
- Usalama
- Ubora wa bidhaa/huduma
Wateja wako wananunua wakati gani?
- Asubuhi, mchana au jioni
- Mwanzoni au mwishoni mwa juma
- Mwanzoni au mwishoni mwa mwaka
Ni wanunuzi wa aina gani?
- Kiasi wanachonunua kwa kipindi fulani
- Mara ngapi wanakuja
- Wanapenda kukopa au wanalipa moja kwa moja
Biashara gani utauza kwa mwezi?
- Biashara yako inashindana na nani na wako wapi hao unaoshindana nao?
- Je wanaathiri biashara yako?
- Je nini kinachokupa nafuu kwako?
- Bei zao.
- Kipimo wanachofunga (kikubwa au kidogo)
- Masharti yao.
Je bei zako utapangaje?
- Utafuata bei za serikali?
- Utaangalia bei wanazouzia wafanyabiashara wengine?
- Utakadiria bei mwenyewe kulingana na gharama?
- Utaweza kupunguza bei au itakuwa haibadiliki?
- Utaratibu gani utatumia kukopesha?
- Mtu akinunua bidhaa nyingi, je atapunguziwa bei?
Kulielewa soko lako
- Unapoingia kwenye biashara, ni vyema kutathmini soko. Hii itakusaidia kujua kama kuna soko
- la bidhaa unayozalisha au huduma unazotarajia kutoa.
Ni nani wateja wako wa sasa na ni nani ambao ni wa uhakika kwako
- Wateja wako ni watu wa aina gani? Kwa mfano umri wao, kipato na elimu yao, vitu wanavyopenda
- na mahitaji yao.
- Wanaishi wapi, na wanapendela kununua nini?
Kuitangaza biashara
- Kuitangaza biashara ni muhimu ili kupata wateja. Matangazo husaidia katika kumtambulisha
- mfanyabiashara mwenyewe na kuifanya biashara itambuliwe na umma.
Uwezekano wa kuongeza kiwango cha mauzo pamoja na mapato upo haswa kwa kutumia matangazo kupitia vyombo vya habari, mbao za matangazo, vitini na vijitabu vyenye kurasa chache.
Lengo kuu la kuvitumia vyombo vya habari ni kuongeza mauzo na mwishowe faida ya biashara.
Nimeipenda xana naminataka nianzishe Duka
LikeLike