Sehemu ya Kumi – Ujasiriamali | Mchanganuo wa Biashara na Umuhimu wake!

308577_10201144942332246_1431798451_n

Jinsi ya Kuanzisha Biashara

Mchanganuo wa biashara na umuhimu wake

Mchanganuo wa biashara ni muhimu sana kufanywa na Wajasiriamali ili kuwezesha biashara zao kufanikiwa. Kuwa na mchanganuo wa biashara huwafanya kuweza kuthibitisha uhalali wa kupata mkopo pale wanapouhitaji, kupata wawekezaji wa kushirikiana nao pia kutambua kama wanapata faida au hasara. Mchanganuo wa biashara pia humwezesha Mjasiriamali kuweka mambo yake vizuri zaidi kabla ya kuanzisha biashara.

Utayarishaji wa mchanganuo wa biashara

Ili kufanikisha utayarishaji wa mchanganuo wa biashara ni sharti kutoa kipaumble kwenye maeneo muhimu yafuatayo:

 • Taarifa binafsi za mjasiriamali.
 • Aina ya biashara itakayofanyika (huduma au bidhaa)
 • Mahali itakapofanyika.
 • Soko linalokusudiwa.
 • Kuwa na taarifa kuhusu watafutaji wengine wanaotoa huduma kwenye soko linalokusudiwa.
 • Mkakati utakaoiwezesha biashara hiyo ifanikiwe.
 • Mahitaji ya fedha, makadirio ya mauzo na gharama za uendeshaji.
 • Jumla ya wataalam watakaohitajika.
 • Chanzo cha mtaji wako kuendesha biashara hiyo – Je, ni kukopa; akiba yako; ubia n.k.

Vipengele vya mchanganuo wa biashara

Mchanganuo wa biashara lazima utimize yafuatayo:

 • Ueleze ni biashara gani unafanya
 • Kwa ajili ya soko gani (wateja ni nani)
 • Ni nani wanaohudumiwa kwa sasa
 • Una mkakati gani wa kuwapata wateja hao
 • Utekelezaji wake utakuwaje
 • Je fedha zitatumikaje kukidhi mahitaji ya biashara.

Faida ya mchanganuo wa biashara

Mchanganuo wa biashara utakuwezesha:

 • Kujua kama bidhaa au huduma yako itanunuliwa.
 • Kujua watu wengine wanaofanya sawa na wewe unachotaka kufanya, wanafanyaje.
 • Kujua kama kulingana na gharama zitakazoingia, bei utakayopanga itakuwa katika uwezo wa wateja wako.
 • Kuona kama unapata faida au hasara.
 • Kujua wapi panahitaji marekebisho.
 • Kurahisisha utekelezaji
 • Benki kuona umuhimu wa kukopesha.
 • Kupanga vizuri mipango ya baadaye hivyo kukupa maono ya uelekeako.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.