Mada ya 1: Ufugaji wa Kuku | Faida za Ufugaji wa Kuku wa Asili

jogooFaida za Ufugaji wa Kuku wa Asili

 • Chakula – nyama ya kuku na mayai hutumika kama chakula muhimu cha wanadamu, chenye protini.
 • Chanzo cha kipato – mkulima hupata fedha akiuza kuku au mayai.
 • Chanzo cha ajira – ufugaji wa kuku hutoa ajira kwa jamii.
 • Kuku hutumika kwenye shughuli za ndoa kama vile kutoa mahari na pia ni kitoweo muhimu katika sherehe hizo.
 • Gharama nafuu za kuanzisha na kuendesha mradi huu.
 • Ni kitoweo rahisi na chepesi kwa wageni kuliko wanyama wakubwa kama ng’ombe au mbuzi.
 • Ni kitoweo kisichohitaji hifadhi, hutumika mlo mmoja au miwili na kumalizika.
 • Kuku na mayai hutumika kwa tiba za asili.
 • Jogoo hutumika kama saa anapowika nyakati za alfajiri na majira mengine ya siku.
 • Hutuhabarisha iwapo kuna kiumbe kigeni au cha hatari kwa mlio maalum wa kuashiria hatari.
 • Mbolea – kinyesi cha kuku kinaweza kutumika katika kurutubisha mashamba ya mazao na mabwawa ya samaki.
 • Kuendeleza kizazi cha kuku wa asili hapa nchini.
 • Soko lipo la uhakika ukilinganisha na kuku wa kisasa kwani nyama na mayai yake hupendwa zaidi na walaji.
 • Manyoya ya kuku hutumika kama mapambo, pia huweza kutumika kutengenezea mito ya kulalia na kukalia.
 • Shughuli za utafiti – kuku wanatumika katika tafiti nyingi za baiolojia kama kutambua mambo ya lishe.
 • Shughuli za viwandani:
  • Mayai yenye mbegu ya jogoo hutumika katika kutengeneza dawa za chanjo.
  • Magamba ya mayai yanaweza kutumika katika utengenezaji wa vyakula vya wanyama.
  • Kiini cha njano cha mayai kinaweza kutumika kutengeneza mafuta ya kuoshea nywele (shampoo).

Upungufu ya Kuku wa Asili:

 • Hutaga mayai madogo yenye wastani wa gramu 47 ambapo kuku wa kisasa hutanga mayai yenye wastani wa gramu 55; aidha hutaga mayai machache wastani wa mayai 60 kwa mwaka ambapo kuku wa kisasa huweza kutaga hadi mayai 300 kwa mwaka.
 • Ukuaji wa taratibu – kuku wa asili hukua taratibu kutokana na lishe duni. Kutokana na hali hiyo kuku huchukua muda mrefu (miezi sita) kufikia uzito wa kuchinjwa (kilo 1 – 1.5). Hali hii pia hufanya faida ya ufugaji wa kuku wa asili kuchukua muda mrefu kupatikana.
 • Nyama yake ni ngumu (huchukua muda mrefu kuiva) ikilinganishwa na kuku wa kisasa.

Changamoto katika ufugaji kuku wa asili:

 • Mabanda: Ukosefu wa mabanda bora.
 • Wezi, wanyama na ndege hushambulia kuku.
 • Magonjwa kama mdondo na ndui huathiri ufugaji wa kuku.
 • Tabia na miiko ya baadhi ya jamii. Baadhi ya jamii za makabila hapa nchini huona ufugaji wa kuku kama ni kitu duni.
 • Upatikanaji haba wa chanjo za magonjwa kama vile, mdondo, ndui, homa ya matumbo.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.