Mada ya 1: Ufugaji wa Kuku | Sifa, Faida na Changamoto za Ufugaji wa Kuku wa Asili

kukuu

Kuku wa Asili ni wale ambao wamekuwepo hapa nchini kwa miaka mingi na damu yao

haijachanganyika na ya kuku wa kigeni. Kuku hawa wana rangi na maumbo mbali mbali.

Idadi ya kuku wa Asili hapa Tanzania inakadiriwa kufikia milioni 56. Kati ya kaya milioni 3.8 zinazojishughulisha na kilimo nchini, kaya milioni 2.3 hujishughulisha na ufugaji wa kuku wa Asili.

Kwa kawaida ufugaji wa kuku wa Asili hapa nchini kwetu Tanzania hufanywa na wafugaji wadogo wadogo wanaoishi kando kando ya miji na wale wanaoishi vijijini. Kuku hawa hufugwa huria (freerange), yaani hufungiwa ndani nyakati za usiku na hufunguliwa asubuhi ili wajitafutie chakula.

Kuku hawa hutoa mazao machache sana yaani nyama na mayai, kwa mfano kuku mmoja hutaga kiasi cha mayai 40-60 kwa mwaka badala ya 100-150 iwapo atatunzwa vizuri. Pia uzito wa kuku hai ni wa chini sana, wastani wa kilo 1.0–1.5 katika umri wa zaidi ya miezi 6 badala ya kilo 1.8 – 2.5 iwapo atatunzwa vizuri.

Sifa za Kuku wa Asili:

  • Wastahimilivu wa magonjwa, lakini ni muhimu wakikingwa na baadhi ya magonjwa ya kuku kama mdondo, ndui ya kuku nk. ili kuweza kuwaendeleza.
  • Wana uwezo wa kujitafutia chakula ardhini, lakini ili kuwaendeleza ni lazima kuwapa chakula bora cha ziada.
  • Wana uwezo wa kuatamia mayai, kutotoa, kulea vifaranga na ustahimilivu wa mazingira magumu (ukame, baridi nk).
  • Nyama na mayai yake vina ladha nzuri kuliko kuku wa kisasa.
  • Kwa kiasi fulani wana uwezo wa kujilinda na maadui kama vile mwewe.
  • Pamoja na sifa hizi ni muhimu kuku hao wakapewa matunzo mazuri, wawekwe kwenye mabanda mazuri na imara, pia wapewe maji na chakula cha kutosha.

 

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

2 thoughts on “Mada ya 1: Ufugaji wa Kuku | Sifa, Faida na Changamoto za Ufugaji wa Kuku wa Asili

  1. mm nafuga kuku chotara pindi wanpokula chakula wanashiba sasa nahitaji kujua ni ugonjwa gani ambao unawashika baadhi ya kuku kuishiwa nguvu

    Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.