Mada ya 2: Ufugaji wa Kuku | Kabila za Kuku wa Asili

dfdgfSi rahisi kuweza kupata kabila halisi (Pure breed) au kizazi halisi (Pure line) za kuku wa Asili kutokana na mazingira ya muingiliano wa vizazi kati ya aina mbalimbali za kuku hao. Hata hivyo kuku hawa wana tofauti za kimaumbile zilizosababisha kuwepo kwa kabila mbalimbali baina yao.

Kabila hizi pia zinahusishwa kwa kiasi kikubwa na eneo kuku hao wanakotoka.

Kutokana na muingiliano wa vizazi, maumbile hayo yanaweza yakajitokeza kwenye aina mbalimbali za kuku, ikiwa na maana kwamba kuku mmoja kuwa na kabila moja au zaidi kwa mara moja. Hivyo aina za kuku zifuatazo zinaweza kutambuliwa kama ndiyo kabila za kuku wa Asili kulingana na maumbile yao na maeneo wanakotoka.

 • Kuchi

Ni kuku wakubwa kwa umbo, warefu na wenye kusimama mgongo ukiwa wima. Kuchi wana manyoya machache mwilini hasa kifuani, wana mdomo mfupi na panga/vilemba vyao ni vidogo. Majogoo huwa na wastani wa uzito wa kilo 3.5 na mitetea kilo 2. Mayai ya kuchi yana uzito wa wastani wa gramu 45. Kuku hawa wanapatikana kwa wingi maeneo ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na Zanzibar. Kuku hawa ni wazuri kwa nyama.

 • Umbo la Kati

Kuku hawa ndiyo hasa wanaoitwa kuku wa kienyeji (wa kawaida). Uzito – Majogoo wastani kilo 1.9, Mitetea wastani wa kilo 1.1, Mayai yana wastani wa gramu 43. Kuku hawa hupatikana sehemu zote za nchi na rangi ya manyoya yao ni mchanganyiko. Kwa kawaida wanaonekana kuwa na uzito mdogo kwa sababu kuna tofauti kubwa sana baina ya ukubwa wa kundi la aina hii. Utafiti umeonyesha kwamba kuku hawa hukua upesi na pia hupata kinga upesi baada ya kuwachanja dhidi ya ugonjwa wa Mdondo (New Castle disease).

 • Ching’wekwe

Kuku hawa hutaga mayai mengi sana kuliko aina nyingine ya kuku wa Asili waliopo Tanzania kwa hiyo wanafaa sana kwa biashara ya mayai. Kuku hawa wenye umbo dogo na wafupi hupatikana zaidi sehemu ya Chakwale mkoani Morogoro na pia sehemu za Umasaini. Uzito – Majogoo wastani wa kilo 1.6 na Mitetea wastani wa kilo 1.2. Mayai yana wastani wa gramu 37.

 • Singamagazi

Kuku hawa wana utambulisho maalum kutokana na rangi zao, kwani majogoo huwa na rangi ya moto na mitetea huwa na rangi ya nyuki. Ni aina ya kuku wakubwa wa asili wanaopatikana zaidi maeneo ya Tabora. Uzito – Majogoo wastani wa kilo 2.9 na Mitetea wastani wa kilo 2.0. Mayai yana wastani wa gramu 56. Kuku hawa ni mbegu nzuri kwa uzalishaji wa mayai na nyama.

 • Mbeya

Rangi ya manyoya ya kuku hawa ni nyeusi au bluu iliyokolea. Uwezo wao wa kuatamia mayai na kuangua ni mdogo sana ukilinganisha na kuku wengine. Uzito – Majogoo wastani wa kilo 3 na Mitetea kilo 2.0. Mayai yana wastani wa gramu 49. Kuku hawa

wanapatikana Ileje mkoani Mbeya, lakini asili haswa ya kuku hawa ni nchi jirani ya Malawi. Hata hivyo, si wa kienyeji asilia bali wana damu ya kuku wa kisasa aina ya ‘Black Australorp’.

 • Pemba

Wana maumbo ya wastani na miili yao ni myembamba. Kuku hawa wanapatikana maeneo mbalimbali ya kisiwa cha Pemba. Rangi ya manyoya yao ni mchanganyiko, panga na vilemba vyao ni vidogo. Uzito – Majogoo wastani wa kilo 1.5 na Mitetea wastani wa kilo 1.0. Mayai yana wastani wa gramu 42.

 • Unguja

Hawana tofauti kubwa sana na wale wa Pemba isipokuwa panga / vilemba vyao ni mchanganyiko kati ya vidogo na vikubwa. Kuku hawa wanapatikana maeneo mbalimbali ya kisiwa cha unguja. Uzito – Majogoo wastani kilo 1.6 na Mitetea wastani wa kilo 1.2. Mayai yana wastani wa gramu 42.

Kuku hawa wa Unguja na Pemba wanashabihiana sana na Kuchi isipokuwa kuku hawa (Unguja na Pemba) ni wadogo.

 • Aina nyingine

Kuna aina nyingine za kuku wa asili wanaotambuliwa kwa muonekano wao. Kuku hawa hupatikana sehemu mbalimbali za Tanzania lakini bado hawajaweza kuainishwa vizuri ili kuweza kutambua sifa zao. Kuku hawa ni pamoja na:

 • Kishingo – Kuku wasio na manyoya shingoni.
 • Njachama au Nungunungu – wenye manyoya yaliyosimama.
 • Kibwenzi – Wenye manyoya mengi kichwani.
 • Kibutu – wasio na manyoya mkiani.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

3 thoughts on “Mada ya 2: Ufugaji wa Kuku | Kabila za Kuku wa Asili

 1. Nashukuru kwa kutujulisha a in a za kuku,ila hujasema namna gani naweza kuwapata,pia ungesema upon mkoa gani,
  Ni kweli kuku kimahesabu kwa haraka wanalipa na wanaweza kumpa MTU ukichaa kwa hesabu take .lakini asikurupuke asije laumu.
  Huyo jamaa anaesema kwa habari ya lishe ajaribu kusoma blogu mbalimbali.lakini watamtajia vyakula lakini hawsemi jinsi ya kutengeneza .
  Kwa uzoefu wangu ni kwamba kuna machine za kubaraza vyakula ,hii niliona na tulitumia pale MBEYA kwani kuna chekeche ya vifaranga,kati na wakubwa .
  Chakula kikibarazwa kwa saizi kulingana na kuku wako ndio unachanganya na halo tayari kwa kulisha kuku wako.
  Mchanganyo huu hujumuisha,;mashudu,pumba,nafaka km mahindi,chokaa,mifupa,premix,unaweza nogesha na vikorokoro kama dagaa,uduvi(from Dodoma) usisahau vitamin(majani) au duif it an huuzwa.
  Kama upon kijijini na machine za kubaraza mashudu ,dagaa,na nafaka hazipo basis mi nitakufundisha kwa njia ya kubaraza kiubunifu ninavyotumia Mimi maana nipo Tabora kjkazi na nimeanza mautundu ya kuongeza kipato kwa ufugaji kuku Wa kienyeji.wasiliana nami kwa 0618940876 (hapa bipu kwa tigo napiga) au +255755754391 hapa piga.kazi njema

  Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.