Maandalizi ya Ufundishaji | AZIMIO LA KAZI

Happybirthday Jiandae_2_3

Azimio la Kazi ni nini?

Azimio la kazi ni mpangilio au utaratibu unaomwezesha mwalimu kuchanganua muhtasari wa somo, kupanga mada na jinsi atakavyozifundisha katika kipindi cha wiki, mwezi na muhula.

Azimio la kazi huonesha pia njia na mbinu atakazotumia mwalimu katika ufundishaji wake katika kila mada, na vifaa atakavyohitaji.

Kwa ujumla –  azimio la kazi ni mpango wa ufundishaji kwa kipindi fulani (kwa muhula au mwaka mzima).

Umuhimu wa Azimio la Kazi

  1. Kuandaa andalio la somo kunahitaji rejea ya azimio la kazi
  2. Ufundishaji unahitaji kwenda na mtiririko mzuri wa mada
  3. Kutoa nafasi ya kufanya marekebisho ya mwelekeo inapobidi
  4. Huonesha wapi mwalimu alipofikia hivyo kumpa nafasi mwalimu anayempokea somo lake kujua pa kuanzia
  5. Huonesha zana na vifaa vya kumsaidia mwalimu katika ufundishaji wake
  6. Humuonesha mwalimu muda wa kufundisha kila mada
  7. Huonesha malengo ya ufundishaji wa somo hilo katika muda aliopanga na jinsi alivyojitahidi kuendana na muda huo

Kumbuka: Azimio la Kazi ni nguzo muhimu sana katika maandalizi yako ya ufundishaji.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “Maandalizi ya Ufundishaji | AZIMIO LA KAZI

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.