Upimaji na Tathmini | Maswali na Majibu

Elimu bora inazingatia Nini hasa
Elimu bora inazingatia Nini hasa
 1.        Andika madhumuni matatu ya tathmini ya kielimu.
 •        Kutaka kujua ufanisi wa mipango ya elimu ili kuweza kurekebisha matatizo yaliyopo, na kama ni mradi-jaribio, kuweza kuamua kutokuendelea nao au kuutekeleza kwa nchi nzima.
 •        Kupata taarifa zitakazosaidia katika kufanya maamuzi ya kuaminika kuhusu mipango ya elimu nchini.
 •        Kuhakikisha kwamba muda, nguvu na jitihada zilizowekwa kwenye mipango ya elimu hazipotei au kutumika vibaya.

 

 1.        Fafanua hatua utakazofuata ili kutathmini somo ambalo unalifahamu maudhui yake barabara.

Ili mwalimu aweze kufanya tathmini nzuri ya somo, inampasa afuate hatua zifuatazo:-

 •          Chunguza malengo mahsusi ya somo lako.
 •          Chunguza kushiriki na uwezo wa wanafunzi darasani wakati wa ufundishaji katika kujibu maswali, majadiliano na kazi za vitendo.
 •          Pima kufikiwa kwa malengo ya somo kwa njia ya kuuliza maswali au kutoa zoezi/mazoezi.
 •          Sahihisha zoezi, toa maksi na chunguza matokeo ya mazoezi ili kubaini ni malengo yapi yamefikiwa na yapi hayakufikiwa.
 •          Andika matokeo ya tathmini.
 1.        Ni muhimu kwa mwalimu kufanya tathmini mara tu baada ya kufundisha somo lake darasani. Fafanua hatua za kuandika tathmini nzuri ya somo.
 •          Katika kuandika ripoti ya tathmini ya somo, mwalimu huangalia kufanikiwa au kutofanikiwa kwa malengo mahsusi aliyoyaweka.
 •          Mwalimu lazima aeleze ni wanafunzi wangapi kati ya waliokuwemo darasani wamefanikiwa kutimiza malengo yaliyowekwa.
 •          Pia aoneshe wanafunzi waliofikia malengo, wamefanya hivyo kwa kiwango gani; kwa usahihi zaidi au kwa kiwango cha kawaida.
 •          Aoneshe pia walioshindwa kufikia malengo, na kiwango cha maarifa walichofikia.

Kumbuka: Unaweza kuonesha kwa asilimia pia.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “Upimaji na Tathmini | Maswali na Majibu

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.