VIPENGELE MUHIMU VYA AZIMIO LA KAZI/SOMO

1484026_621894097847301_1384491114_o

Muhula: sehemu hii huandikwa namba ya muhula ambapo azimio la kazi litatumika

Mwezi: huandikwa jina la mwezi ambapo mada fulani zitafundishwa

Ujuzi: ni maarifa, stadi na muelekeo anaoupata mwanafunzi baada ya kujifunza mada husika.

  • Maarifa, ni utambuzi anaoupata mtu au mwanafunzi baada ya kujifunza jambo fulani
  • Stadi, ni ule uwezo wa mwanafunzi kutumia viungo vyake vya mwili kufanya jambo linalotokana na somo alilojifunza, mfano kucheza, kuumba vitu mbalimbali, kufanya majaribio katika maabara, ufaraguzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia.
  • Mielekeo, inahusu mabadiliko yanayohusu stadi za maisha.Hii ni pamoja na mwanafunzi anavyobadili mwelekeowake kutokana na mambo aliyojifunza.

Wiki: sehemu hii huandikwa idadi ya wiki katika mwezi fulani ambapo sehemu fulani ya mada itafundishwa

Idadi ya vipindi: huandikwa idadi ya vipindi watakavyofundishwa katika idadi ya juma au majuma yaliyooneshwa

Mada kuu: hapa huandikwa mada kuu husika kama inavyoonekana katika muhtasari wa somo

Mada ndogo: hapa hujazwa mada ndogo kama ilivyo katika muhtasari wa somo

Vitendo vya ufundishaji: hapa hujazwa vitendo atakavyofanya mwalimu katika kujiandaa kufundisha mada husika na atakavyowashirikisha wanafunzi katika harakati za kufundisha na kujifunza

Vitendo vya ujifunzaji: hapa hujazwa vitendo vitakavyofanywa na wanafunzi kwa maelekezo ya mwalimu. Vitendo hivyo ama ni vya kujiandaa kujifunza katika muhula ufuatao au wakati uliopo wa muhula

Vifaa/zana: katika sehemu hii mwalimu anapaswa kuonesha vifaa au zana mbalimbali atakazotumia wakati waufundishajiwa mada ili kuweza kufanikisha ufundishaji na kuweza kufikia lengo lako mahsusi

Rejea: hapa mwalimu ataonesha vitabu alivyotumia kama rejea katika mada anayofundisha

Maoni: katika safu hii mwalimu atatoa maoni yake kuhusu mafanikio aliyoyaona, matatizo yaliyojitokeza na mapendekezo ya kuboresha ufundishaji

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

4 thoughts on “VIPENGELE MUHIMU VYA AZIMIO LA KAZI/SOMO

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.