Haki za Raia | DHAMANA NI NINI?

DSC01516

Dhamana ni ruhusa ya kuwa huru anayoweza kupewa mtuhumiwa wakati uchunguzi wa kosa lake unaendelea au shauri lake likiendelea kusikilizwa mahakamani, au akisubiri uamuzi wa rufaa yake.

Dhamana ni haki inayopata msingi wake katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ambayo ina dhana inayotamka kwamba mtu hatochukuliwa kuwa mwenye hatia mpaka tuhuma zithibitishwe dhidi yake.

Ili kuzingatia dhana hii ni muhimu kumruhusu mtuhumiwa kwa kumpa dhamana apate kuwa nje ya kizuizi mpaka hapo tuhuma zake zitakapothibitishwa na mahakama. Kwa mantiki hii dhamana ni haki ya mtuhumiwa na wala sio upendeleo au zawadi.

Nani hutoa Dhamana?

Dhamana huweza kutolewa na:-

(i) Jaji au Hakimu

(ii)  Mkuu wa kituo cha polisi ambapo mtuhumiwa ameshikiliwa.

Yapo makosa ambayo kisheiria hayaruhusu dhamana, nayo ni:

I. Kosa la kuua kwa kukusudia

II. Kosa la uhaini

III. kosa la unyang’anyi kwa kutumia silaha

IV. Kosa la ugaidi

V. Kosa la kunajisi

Mtuhumiwa anaweza kukosa dhamana kutokana na mazingira yafuatayo:

(i) Mtuhumiwa alishapewa dhamana akaikiuka.

(ii) Kwa mahitaji ya  usalama wa mtuhumiwa mwenyewe

(iii) Kwa usalama wa jamii

(iv) Kwa kuchelea kumwachia nafasi ya Kuvuruga upelelezi

(v) Sababu nyingine kama atakavyoona Mkuu wa kituo

Aina za Dhamana:

Dhamana zipo za aina zifuatazo:-

(i) Dhamana ya mkataba wa maandishi:

Huu ni mkataba kati ya mtuhumiwa au mdhamini kujifunga kwamba mtuhumiwa atahudhuria Baraza la mahakama siku iliyotajwa. Iwapo mtuhumiwa asipotokea mdhamini huyo atalazimika kutekeleza masharti fulani au hata kifungo.

(ii) Dhamana ya Mali:

Iwapo mtu hana kiasi cha fedha, anaweza kuweka dhamana kwa kukabidhi mali zake zinazohamishika.

(iii) Dhamana ya kutambuliwa:

Aina hii ya dhamana humtaka mtuhumiwa au mdhamini kuweka sahihi ikiwa masharti ya mkataba wa dhamana yamevunjwa.  Aina hii huonekana kama yenye unafuu kidogo.

(iv) Dhamana ya kuweka fedha:

Hii ni aina ya dhamana ambapo, mtuhumiwa, rafiki au ndugu hutakiwa kutoa kiwango fulani cha fedha na iwapo hatahudhuria mahakamani fedha hiyo hutaifishwa na serikali.

Nani anaweza kuomba dhamana?

 •   Mshtakiwa
 •   Ndugu au rafiki wa mshtakiwa
 •   Wakili wa mshtakiwa

Wakati wa kuomba dhamana:

 •   Muda wowote wakati kesi inaendelea na wakati rufaa ikisubiriwa
 •   Wakati mashtaka yanaandaliwa na polisi au kabla ya hukumu kutolewa au rufaa kuamuliwa

 

KUMBUKA

Dhamana ni haki ya kikatiba ya kila mtuhumiwa, kwa hiyo mtuhumiwa ana haki ya kuomba dhamana wakati wowote kabla hajapatikana na hatia au baada ya kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa dhidi yake. Pia dhamana ya polisi haihusishi fedha taslimu, na hutolewa bure. Ni kosa kubwa kwa askari polisi kupokea fedha/rushwa katika zoezi la utoaji wa dhamana na katika utendaji kazi wake.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

2 thoughts on “Haki za Raia | DHAMANA NI NINI?

 1. napenda kufahamu, sifa zipi za mtu kuweza kupata dhamana?
  pia nikiwa nakibar cha kusachi MTU sheria itanibana endapo nitakosa kidhiti?

  Like

 2. kwa maoni yangu hapa kwetu polisi wanakuwa wagumu sana kutoa dhamana ktk maana hlisi ya haki ya mtuhumiwa kupewa dhamana,kuna kuwa na sabau na mizunguko mingi inayokatisha tamaa,heri mahakamani na si polisi,ushahidi upo wa kutosha.

  Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.