Kutenganisha au kuvunja Ndoa

970058_271886582987042_567024685_n (1)

 

Kutengana

Hii ni hatua ya mwanamke na mwanaume kuishi tofauti ingawa bado ndoa yao haijavunjwa  bali kwa sababu ya kutoelewana katika maisha yao ya ndoa. Kutengana katika maisha ya ndoa kunaweza kuwa kwa makubaliano kati ya wanandoa au kwa amri ya Mahakama.

Kuvunja Ndoa

Ndoa inaweza kuvunjwa tu na vitu viwili navyo ni

I.      Amri ya mahakama

II.      Kifo cha mmoja wa wanandoa

Iwapo wanandoa wanataka kuvunja ndoa ipo sababu inayokubalika kisheria inayoweza kuifanya  Mahakama kufikia uamuzi  wa kutoa  amri ya kuvunja ndoa.  Sababu hiyo  ni:-

Ndoa  iwe imefikia hatua ya kutoweza kurekebishika kabisa.  Mfano: pale wanandoa watakapoonyesha hawawezi kuishi pamoja kama mke na mume.

Katika kudhibitisha hali hii ushahidi wa mambo yafuatayo waweza kutolewa mahakamani:

I.      Ugomvi wa mara zaidi ya moja na kuonya.

II.      Iwapo mmojawapo anamfanya mwenzie tendo kinyume na maumbile.

III.      Ukatili.

IV.      Kutojali kwa makusudi

V.      Kutelekeza

VI.      Kutengana kwa hiari

VII.      Kifungo cha muda mrefu (kama miaka mitano na zaidi).

VIII.      Ugonjwa wa akili,

IX.      uhanithi,

X.      kifafa

XI.      Iwapo mmoja atabadili dini.

Taratibu za kuomba Mahakama kuvunja  Ndoa:

Mmojawapo kati ya wanandoa anaweza kupeleka ombi la kuvunja ndoa mahakamani  iwapo  mambo yaliyotajwa hapo juu yametokea. Zifuatazo ni hatua za kuchukua

Hatua ya 1

Muombaji atapeleka maombi au malalamiko yake katika Baraza la usuluhishi.  Mabaraza ya usuluhishi yanaweza kuwa Baraza la Dini (kama Bakwata), Baraza la Kata au Baraza la Usuluhishi wa Ndoa la Kamishna wa Ustawi wa Jamii.

Hatua ya 2

Baraza la usuluhishi litajaribu kusuluhisha mgogoro ili  ndoa isivunjike kwa kuwakutanisha wanandoa na kuwasuluhisha.

Hatua ya 3

Iwapo Baraza litashindwa kusuluhisha na likiridhika kwamba ndoa hiyo haisuluhishiki basi  Baraza litatoa Hati inayoonyesha kwamba limeshindwa kusuluhisha na inyouelekeza  mgogoro ule mahakamani.

Hatua ya 4

Mwombaji atapeleka shauri la kuomba kuvunja ndoa katika Mahakama yenye uwezo huo. Katika maombi hayo, muombaji anaweza pia kuomba mambo mengine yafuatayo:-

I.      amri ya matunzo.

II.      ulinzi na matunzo ya watoto wa ndoa.

III.      mgawanyo wa mali zilizopatikana  ndani ya ndoa.

Hatua ya 5

Mahakama ikiridhika kwamba masharti yote yametimia itapokea maombi ya mwombaji na taratibu za kujulisha wahusika wote zikikamilika, mahakama itasikiliza ushahidi wa pande zote na iwapo itaridhika na sababu zilizotolewa katika ushahidi itatoa amri ya kuvunja ndoa, na amri nyingine kama itakavyoona inafaa.

 

KUMBUKA:Kuna aina ya talaka ambazo hutolewa kienyeji na wanandoa wa kiislamu kama zile zijulikanazo kama talaka moja, talaka mbili, talaka rejea au talaka tatu; Talaka hizi hazivunji ndoa kisheria bali huwa ni ushahidi tu wa nia kuonyesha kwamba wanandoa wanataka kuachana.  Mahakama inaweza kupokea aina hii kama ushahidi tu lakini sio kama tamko lililovunja ndoa.

 

 

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.