Namna  Mbalimbali za Kufunga Ndoa

 

Mateno Ramadhani
Ndoa ya Kiisalmu

Sheria ya Tanzania inatambua namna  zifuatazo za ufungaji ndoa:

(i)                  Kidini: hii ni ndoa inayofungwa baina ya wanandoa wakristo, waislamu au wa dini nyingine kwa taratibu za dini na madhehebu yao.

(ii)                Kimila: kwa kufuata mila na tamaduni za jamii husika.

(iii)               Kiserikali: Hii hufungwa mbele ya ofisa wa serikali mwenye mamlaka ya kufungisha ndoa kwa kufuata taratibu zilizoainishwa na sheria ya ndoa.

Dhana ya ndoa

Kisheria  mwanamke na mwanamume walioishi pamoja kama mke na mume   kwa kipindi cha muda usiopungua miaka miwili japo hawakufunga ndoa kwa namna yoyote iliyoelezwa hapo juu huchukuliwa kama mke na mume .Dhana hii hata hivyo husimama pale ambapo hakuna mmoja kati ya wenzi hao wawili ambaye alikuwa ndoa inayoendelea wakati akiingia katika mahusiano hayo.

Hii ni dhana inayoweza kukanushika ikiwa mmoja wao atatoa ushahidi wa kuonyesha kuwa wenzi hao hawakuishi katika paa moja kama mke na mume au alikuwa na ndoa nyingine iliyokuwa ikiendelea

Sifa za Wanandoa

I.      Umri, kwa mwanamke: umri wa chini wa kufunga ndoa  kwa hiari yake mwenyewe tu ni  miaka 18 na kwa mwanaume ni miaka 18 na iwapo itabidi kuoana kabla ya umri  wa miaka 18 kwa msichana  basi itabidi apate idhini ya wazazi ikiwa ametimiza miaka 15 na iwapo ana miaka 14 itabidi apate idhini ya  Mahakama.

II.      Hiari: Lazima kila mmoja awe ameridhia kwa hiari yake kamili bila hila, kulaghaiwa au kulazimishwa na mtu yoyote.

III.      Jinsi, lazima wawe watu wawili wa jinsi tofauti, mmoja wa kiume na mwingine wa kike.

IV.      Wasiwe maharimu yaani wasiwe na undugu wa damu.

V.      Mke asiwe katika eda yaani miezi mitatu toka alipoachwa au kufiwa na mume

VI.      Pingamizi:Wanaotazamia kufunga ndoa wasiwe wamewekewa pingamizi

KUMBUKA:

 Jamii kadhaa hapa nchini zina utamaduni wa kuwalazimisha vijana kufunga ndoa kama adhabu dhidi ya tabia zao za kufanya mapenzi kabla ya ndoa au kama suluhisho la kukwepa “aibu” ya watoto wao kuzaa kabla ya ndoa.Katika jamii za pwani ndoa hizi hujulikana kama ndoa za mikeka na hufungwa kwa lazima bila kujali ridhaa ya wahusika.

Ikumbukwe kuwa ndoa zilizofungwa kwa mtindo huu ni batili kisheria kwa vile waliofungishwa ndoa hawakuridhia jambo hilo.Pia ni kitendo cha ukandamizaji kwa vijana kwa vile wanalazimishwa kuingia katika makubaliano yanayokusudiwa kudumu maisha yao yote bila kujali kama wamehiari hivyo au hapan

 

KUMBUKA:

Jamii kadhaa hapa nchini zina utamaduni wa kuwalazimisha vijana kufunga ndoa kama adhabu dhidi ya tabia zao za kufanya mapenzi kabla ya ndoa au kama suluhisho la kukwepa “aibu” ya watoto wao kuzaa kabla ya ndoa.Katika jamii za pwani ndoa hizi hujulikana kama ndoa za mikeka na hufungwa kwa lazima bila kujali ridhaa ya wahusika.

Ikumbukwe kuwa ndoa zilizofungwa kwa mtindo huu ni batili kisheria kwa vile waliofungishwa ndoa hawakuridhia jambo hilo.Pia ni kitendo cha ukandamizaji kwa vijana kwa vile wanalazimishwa kuingia katika makubaliano yanayokusudiwa kudumu maisha yao yote bila kujali kama wamehiari hivyo au hapana.

Ndoa iliyofungwa yaweza kubatilishwa iwapo

I. Ilifungwa wakati ambapo mwanandoa alikuwa na ndoa nyingine wakati huo iliyokuwa ikiendelea.

II. Kama ilikuwa ndoa ya ndani ya dini moja, mmoja wa wanandoa ameamua kubadili dini.

III. Mmoja wa wanandoa anapokataa kutimiza moja ya masharti ya ndoa, kama vile kukataa kushiriki tendo la ndoa.

IV. Mmojawapo anapothibitika kuwa na magonjwa ya zinaa ya muda mrefu yasiyopona.

V. Iwapo mke alipata mimba ya nje wakati alipokuwa anafunga ndoa.

Haki na Wajibu katika Ndoa

Katika ndoa kila mmoja ana haki na wajibu katika:

I. Kushiriki tendo la ndoa

II. Kuzaa watoto

III. Mke kupata matunzo kutoka kwa mume na kinyume chake pale ambapo mume hana uwezo kwa sababu ya ugonjwa au ulemavu.

IV. Kumiliki mali (ya ndoa na binafsi)

V. Mke kukopa kwa dhamana ya mumewe

VI. Kutunza siri za unyumba

VII. Haki ya kuishi katika nyumba ya ndoa

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “Namna  Mbalimbali za Kufunga Ndoa

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.