VIPENGELE MUHIMU VYA ANDALIO LA SOMO

1502751_613539485349429_1975245874_o

Katika kuandaa Andalio la Somo yampasa mwalimu kuzingatie vipengele muhimu vifuatavyo;

 1. Jina la somo
 2. Tarehe, darasa, muda wa kipindi, idadi ya wanafunzi
 3. Mada kuu na mada ndogo
 4. Malengo ya somo
 5. Vifaa vya kufundishia na kujifunzia
 6. Vitabu vya rejea
 7. Uwasilishaji wa somo hatua kwa hatua
 8. Kazi za mwalimu na za wanafunzi
 9. Maoni kuhusu mafanikio/matatizo ya ufundishaji wa kipindi
 10. Tathmini
 11. Mazoezi ya wanafunzi

         

a)      Vipengele 1, 2 na 3: 

Vinamsaidia mwalimu kuwa na kumbukumbu ya vipindi vilivyofundishwa kwa mwaka katika somo husika.

b)      Malengo ya somo:

Haya ni malengo Mahususi yaani yanayopimika – yanaonesha matarajio aliyo nayo mwalimu kwa wanafunzi wake baada ya kipindi au somo. Mfano mwanafunzi aweze kutaja, kuandika au kusoma kitu Fulani kwa kiwango Fulani cha ufanisi

c)      Vifaa vya kufundishia:

Hizi ni zana ambazo mwalimu anatarajia kuzitumia katika kufundisha somo husika.

d)      Vitabu vya rejea:

Hivi ni vitabu ambavyo mwalimu huvisoma ili kupata marifa, stadi nk. Vitabu vya rejea hujumuisha pia majarida na maandiko mengine ambayo hutumika kuandaa somo

e)      Uwasilishaji wa somo hatua kwa hatua:

Hapa mwalimu anapaswa kuandika vitu viwili muhimu: kazi na hatua zote atakazofuata mwalimu wakati wa somo, pia atayarishe mawazo/maudhui makuu anayotaka yazingatiwe na wanafunzi.

f)        Kazi za wanafunzi;

Kazi za wanafunzi zinaweza kuwa kuchora, kueleza, kuandika, kujibu maswali ya mwalimu, kufanya maigizo, kujadiliana nk, hakikisha kwa kila kipindi unawapa wanafunzi wako kazi japo ndogo ya kufanya.

g)      Mazoezi ya wanafunzi;

Haya ni maswali ambayo mwalimu huwapa wanafunzi kupima kama malengo ya somo yamefikiwa wakati wa kipindi

h)      Tathmini;

Mwalimu aandike maelezo kama somo limefaanikiwa au la, na kwa kiwango gani.

i)        Maoni;

Mwalimu aeleze hatua za kuchukua kutokana na tathmini ya somo lake. Kwa mfano kama somo halikufanikiwa atalirudia, atarudia baadhi ya vipengele.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

9 thoughts on “VIPENGELE MUHIMU VYA ANDALIO LA SOMO

 1. Asante sana kwa hamasisho hiyo ila Nina swali kuhusu tathmini na maoni.kama nilivyofunzwa sehemu hizi mbili hupatikana katika maazimiyo ya kazi.naomba kuelezwa zaidi ni pate kujua

  Like

 2. Kinpengele F na E hapa ndio nahitaji ufafanuzi mm kama mwalimu ina maana nitakachokifanya nikuandika maswali nkliyotoa darasani au nitaandikia maelezo kwa mfano
  Kazi ya mwl.
  -to provide class-work to students
  Kaz ya mwanafunz
  -are the students should do class work provided by his/her teacher?????????

  Mwongozo please

  Like

  1. Karibu Mwalimu baraka,

   Kwa kila kipengele au hatua ya somo kuna namna yake ya maswali au muongozo utakaouweka wewe mwalimu ili ukuwezeshe kuimarisha maarifa kwa mwanafunzi.

   Mfano hapo ulivyoandika hivyo ni sawa ila hayo maelezo yatafaa kwa hatua ya mwisho (Hitimisho/Conclusion)

   Kwa hatua zingine unaweza kusema mfano;

   Hatua – Utangulizi

   Kazi ya Mwalimu: Kuuliza maswali kuhusiana na somo lililopita (kama ni muendelezo wa somo)

   Kazi ya Mwanafunzi: Kujibu maswali na kushiriki majadiliano ya swali.

   Yapo mambo mengi sana ya kujadili katika hatua mbalimbali za kufundisha hivyo tutajitahidi kuweka mfano wa Andalio la somo lililojazwa ili muone mfano halisi.

   Ahsante sana.

   Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.