Katuni ni nini? Ufasihi wa Katuni | Mbinu za Kufundishia Kiswahili

katuni 2

Neno katuni limetokana na neno la Kiingereza ‘Cartoon’ ambalo nalo limetokana na neno la Kifaransa ‘Cartourche’ lenye maana ya kuchora. Asili ya neno hili ni kwa Warumi/ Waroma ambako liliitwa ‘Cartone’ likiwa na maana ya michoro katika karatasi ngumu

Katuni ni fani iliyotolewa fasili nyingi kulingana na mitazamo ya wataalamu mbalimbali. Katuni ni michoro yoyote iliyochorwa au kupakwa rangi kwa ajili ya kufurahisha, au kutoa maoni ya mhariri au kwa ajili ya matangazo (Encylopaedia ya Grolier Academic 1983:176)Nayo Encyclopaedia ya Americana (1982:728) Juzuu ya tano (5) inaeleza kwamba katuni ni mchoro, kiwakilisho au ishara ambayo husababisha ucheshi, utani au kejeli.

Tunaweza kusema kwa kifupi kuwa katuni ni picha zilizochorwa kisanii ambazo zinatoa ujumbe kiucheshi, kikejeli, kimzaha, na kiramsa.

Katuni mnato ni nini?

Hizi ni Katuni ambazo huchorwa magazetini, na kwenye majarida.

Katuni sogezi ni nini?

Ni zile katuni ambazo zinazooneshwa katika sinema na televisheni.

Je, Fasihi hukamilishwa na nini?

Ni wazi kuwa fasihi kama sanaa itumiayo lugha hujengwa na sura mbili ambazo hutegemeana, hukamilishana na kujengana. Sura hizo mbili ni maudhui na fani ambazo kwa baadhi ya wataalamu, wamefafanua kwamba ni vitu viwili visivyoweza kutenganishwa.

Maudhui hukamilishwa na nini?

Maudhui hukamilishwa na dhamira, ujumbe, migogoro, na falsafa ya mwandishi,

Fani hukamilishwa na nini?

Fani hukamilishwa na muundo, mtindo, mandhari, wahusika na matumizi ya lugha.

Kwa nini tunatumia Katuni kufikisha ujumbe?

Katuni hubeba picha mbalimbali ambazo huwa na maana fiche zinazoweza kufafanuliwa kulingana na upeo wa kifikra na muktadha alionao msomaji.

Kwa nini Katuni zinachukuliwa kama fasihi picha?

King’ei (2005:1) anasema kwamba, sanaa ya kifasihi inatokana na usanifu, ufasaha au ufundi wa kuwasilisha mawazo au fikra za mwanadamu, na nia hasa ya kuwasilisha mawazo kama hayo ni kudhihirisha hali fulani za maisha yake kama vile furaha, huzuni, matatizo, fanaka, utetesi, kashifa, sifa, maelekezo au uchambazi, basi wanakatuni wamewasilisha fikra zao kwa njia ya utani, mzaha, kejeli, dhihaka, ucheshi na ramsa.

katuni

Ucheshi ni nini?

Ucheshi ni mbinu ya kifani ambayo hutumiwa na watambaji fasihi simulizi kwa nia tofauti. Kama ilivyo katika baadhi ya kazi za fasihi andishi, vivyo hivyo katika fasihi simulizi, ucheshi hutumiwa kuwa kipumuo, hasa baada ya matukio ya kutisha, au maelezo marefu yenye kuwachosha wasikilizaji.

Kejeli ni nini?

Kejeli ni usemi ambao maana yake ya ndani ni kinyume chake na inabeuwa maana yake halisi: ni usemi wa kebehi ambao kisemwacho sicho kikusudiwacho na msemaji, kisemwacho kumbe ndicho kinabeuliwa.

Mzaha ni nini?

Mzaha ni masimulizi mafupi ya kuchekesha ambayo uaghalabu hufanywa kupitishia wakati. Baadhi ya mizaha huwa ni ya matusi, baadhi ni ya kejeli au kebehi zenye kusaliti tabia au matendo ya watu fulani.

Nini maana ya ramsa?

Ramsa nimbinu ya kifutuhi inayotawaliwa na ucheshi na kusababisha kicheko cha furaha kinachotoka katika hisia za msomaji baada ya kusoma kazi fulani ya kifasihi.

katuni 3

 

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

3 thoughts on “Katuni ni nini? Ufasihi wa Katuni | Mbinu za Kufundishia Kiswahili

  1. Kutoka Nairobi-Kenya.
    Ahsanteni sana.
    Nimefurahishwa sana na katuni pamoja na maelezo yenye busara na hekima.Mola awaneemesheye na kuwabariki daima magwiji.

    Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.