MISINGI MIKUU YA HAKI ZA BINADAMU

Tanzania@50 1

Misingi ya haki za binadamu ni zile kanuni zinazokubalika kutumika katika tafsiri na utekelezaji wa Haki za Binadamu.  Kanuni hizi zinatuwezesha kuzielewa vizuri na kuzitekeleza kikamilifu haki za binadamu.

Misingi hii ni kama ifuatavyo:

(i) Zimefungamana na utu wa mtu, kila binadamu huzaliwa nazo na hazitolewi wala kugawiwa na mtu au mamlaka yoyote. Ni vielelezo vya thamani ya utu.

(ii) Usawa. Haki za binadamu ziko sawa kwa wote kwa maana hazitakiwi kutolewa kwa ubaguzi wa aina yoyote ile. Hivyo zinazingatia usawa baina ya binadamu wote bila kujali rangi, umbile, dini, kabila, kipato, n.k. mfano haki za binadamu zinazuia uwekaji wa taratibu au masharti ya upendeleo katika fursa au huduma

(iii) Hazigawanyiki na hutegemeana. Haki za binadamu zinahusisha maisha ya kila siku ya binadamu hivyo haki moja inategemea utekelezaji wa haki nyingine; mamlaka yoyote haiwezi kuchagua haki za kutekeleza na zile za kupuuzia. Mfano upatikanaji wa haki zote unategemea haki ya kuishi na vilevile haki ya kuchaguliwa kuwa kiongozi  katika ngazi fulani fulani  inategemeana na haki ya kupata elimu na pia wakati mwingine uhuru wa kujumuika na kushirikiana na wengine unategemea upatikanaji wa uhuru wa kukusanyika.

(iv) Ni za kilimwengu; hii inamaana kwamba haki hizi ni lazima zizingatiwe kuheshimiwa na kulindwa mahali popote ulimwenguni bila kujali mipaka ya nchi, bara n.k. au mila na desturi za mahala, mifumo ya kiutawala au itikadi za kisiasa.

(v) Ushiriki: Huu ni msingi unaotokana na msingi wa usawa na haki ya kuheshimu utu wa mtu mwingine. Hii ina maana kuwa kaama tunaamini watu wote ni sawa na wanastahiki kuheshimiwa, lazima kila mtu ashirikishwe katika kuamua mambo yanayowagusa maslahi yake. Hakuna uhalali wa kumshurutisha mtu mwingine atekeleze maamuzi yanayomhusu bila kumshirikisha katika kufikia maamuzi hayo.

Kwa kifupi hii ndio misingi mikuu ya haki za binadamu kama ambavyo zimetamkwa katika Tamko la Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu.

Ingawa haki hizi za binadamu zinawalinda wanadamu wote bado yapo makundi maalum ambayo yanatakiwa kulindwa kwa namna ya pekee kwa sababu yapo kwenye hatari zaidi ya kuathirika kuliko makundi mengine.  Makundi haya ni pamoja na wanawake na watoto.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “ MISINGI MIKUU YA HAKI ZA BINADAMU

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.