Nini maana ya Jamii?


DSC04958

 1. Nini maana ya jamii

Jamii ni mkusanyiko wa watu wanaoishi kwa pamoja katika eneo moja la kijiografia wakiunganishwa na historia yao na wakitambuliwa kwa utamaduni wao, lugha, mila na desturi.

Mfano makabila mbalimbali ,miundo ya kujitawala wao wenyewe, mfano taifa pamoja na shughuli zao za kiuchumi. Mfano wafugaji au wavuvi, mafunzo na taaluma, mfano jamii ya wanafunzi wa chuo kikuu, n.k

 1. Je, ni vigezo gani vinavyoitambulisha jamii?

Ili mkusanyiko fulani uweze kuitwa Jamii vigezo vifuatavyo lazima viwepo:-

 • Watu wa jinsi na rika zote yaani wanawake kwa wanaume wazee kwa vijana
 • Wanaoishi pamoja, mfano wakazi wa kijiji fulani
 • Ndani ya mipaka ya kieneo mfano wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro
 • Kwa muda fulani unaoweza kuwaunganisha:

-Kiutamaduni mfano mila na desturi za aina moja mathalani kabila la wakurya

-Kiuchumi,mfano aina moja ya uzalishaji mali kama wavuvi,wakulima n.k.

-Kimahusiano yao na taasisi mbalimbali.

 • Lugha inayowatambulisha mfano makabila mbalimbali au mataifa
 • Utaratibu maalum wa kushiriki kutawala au kutawaliwa mfano ufalme fulani  n.k.
 • Makundi ya jamii yenye malengo na mwelekeo mmoja au tofauti lakini unaolenga kuendelea kuishi kama jamii moja mfano watu wa dini au itikadi mbalimbali za kisiasa.
 1. katika Jamii yapo makundi ya aina gani?

Makundi katika jamii hujitokeza kwa namna mbalimbali tofauti:-

yanaweza kujitokeza:

 • Kimaumbile: mfano watu wenye ulemavu na watu wasio na ulemavu
 • Kiuwezo wa uchumi: mfano matajiri na watu wenye kipato cha chini
 • Kimtazamo wa kisiasa: na kijamii mfano wahafidhina na wale wenye mtizamo wa kimamboleo au vyama mbalimbali vya siasa
 • Kimahusiano katika uzalishaji mali: mfano waajiri na waajiriwa

Mahusiano ya makundi hayo yanaweza kuwa:-

 • Yanayoungana na kuelekeana mfano vyama  mbali mbali vya wafanyakazi chini Tanzania
 • Yanayokinzana na kutofautiana mfano vyama vya siasa katika kambi ya  upinzani na chama tawala
 • Yanayojitokeza kwa utashi ,kama mifano iliyotajwa hapo juu
 • Na yanayojitokeza bila utashi.

Aina ya Makundi ya Jamii

Kulingana na namna yanavyojitokeza tunaweza kutambua makundi yafuatayo:-

(i) Makundi yatokanayo na maumbile na rika:-

 • Watoto wadogo.
 • Vijana.
 • Watu wazima na wazee
 • Watu wenye ulemavu

(ii) Makundi yatokanayo na uwezo wa uchumi:-

 • Watu wenye kipato duni
 • Watu wenye uwezo kiuchumi

(iii) Makundi yatokanayo na uwezo wa kielimu

 • Tabaka la wasomi.
 • Na tabaka la wasio na elimu.

(iv) Makundi yatokanayo na mtazamo wa kisiasa na kijamii:-

 • Matabaka ya watawala na watawaliwa
 • Vyama vya kisiasa
 • Vyama vya ushirikiano kijamii
 • Ukabila, ukoo
 • Wanafunzi.

(iv) Makundi yatokanayo na ushirikiano na mahusiano ya uzalishaji mali:

 • Vyama vya wafanyakazi.
 • Wasimamia uzalishaji, wazalishaji
 • Wafanyakazi na wakulima.

Kutokana na aina ya makundi katika jamii ni wazi kwamba, kwa namna mahusiano yanavyojitokeza, baadhi ya makundi haya huwa yako kwenye hatari na urahisi zaidi wa kuathirika au kunyanyasika.  Baadhi ya sababu za kuwa katika hatari zaidi ya kushambuliwa ni kama:-

 • Uwezo mdogo wa kimaumbile wa kuweza kujihami au kujitetea dhidi ya madhara au shambulio la mwili, mathalani watoto wadogo, wazee vikongwe, na wenye ulemavu.
 • Uwezo mdogo wa kiuchumi wa kujihami dhidi ya manyanyaso yatokanayo na hali zao, kama vile umasikini,
 • Uwezo mdogo wa kiufahamu kama wasiojua kusoma na kuandika.

Kwa vipengele hivi basi tunaweza kujumuisha makundi ya jamii yaliyo katika hatari na urahisi zaidi wa kuathiriwa kuwa ni:-

 • Watoto
 • Wanawake
 • vijana
 • Walemavu
 • Wakimbizi
 • Wagonjwa wa ukimwi
 • Wazee wenye umri mkubwa sana

Hata hivyo ndani ya makundi haya bado yapo makundi ya watu ambo urahisi wao wa kuathirika ni mkubwa zaidi kuliko wenzao walio katika makundi hayo mfano :

Katika kundi la watoto: yatima, watoto wenye ulemavu,watoto wasio na uangalizi wa wazazi au walezi mfano watoto waishio mitaani na walio katika ajira mbaya na wale wanaoishi na virusi vya ukimwi.

Katika kundi la wanawake: wajane ,waliotelekezwa,walemavu n.k

Katika kundi la vijana : vijana walio nje ya shule na wasio na ajira au wale walio katika ajra hatarishi mfano wanaojihusisha na ngono ,kazi za migodini ,mashambani na viwandani.

 

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.