ULINZI WA WATOTO

 1274287_578636305506414_1917762441_o

Katika sheria ya mila haswa katika Tangazo la Serikali Nambari 436/63, mwongozo unatolewa juu ya ulinzi wa watoto waliofiwa na baba yao bado wadogo hususan mrithi ambaye hayupo wakati wa kurithi, na ulinzi wa mke na watoto wa mtu anayekwenda safari ndefu.

Katika sehemu hii Baraza la ukoo linapewa uwezo wa kuteua mlinzi wa watoto ambaye atafanya yafuatayo:-

I.      Kuwatunza watoto na mama yao.

II.      Kuangalia mali yao isipotee wala kuharibika.

III.      Kuongoza familia  kwa kushauriana na mama wa watoto kama yupo, juu ya uzalishaji kama vile kilimo, kuozesha watoto wa kike n.k.

IV.      Kusimamia mashauri, malipo ya kodi, ada za shule, kuhudhuria minada ya

mifugo n.k. inayohusiana na nyumba ile.

 Mlinzi hapaswi kufanya yafuatayo:-

  •  Kuuza ardhi wala mimea ya kudumu iliyo chini ya ulinzi wake.
  • Kujilipa mshahara au malipo maalum kwa kazi yake ya ulinzi.

Malalamiko kwa kutokuridhishwa na ulinzi:-

  •  Mlinzi anaweza kulalamikiwa na mama wa watoto, au watoto ndugu mwingine, au watoto wenyewe watakapokua ila mashtaka haya hayatapokelewa na mahakama pasipo kufikishwa kwanza kwa Baraza la Ukoo.

Mwisho wa Ulinzi au Kubadilishwa kwa Ulinzi:-

  • Mrithi wa kwanza akifikia umri wa miaka ishirini na moja (21) au atakapooa (akioa kabla ya kufikia umri huu) na akifaa, anawekwa na baraza la ukoo kuwa mlinzi wa watoto wadogo waliobaki.
  • Watoto wengine vilevile watatoka katika ulinzi watakapofikisha umri wa miaka ishirini na moja au watakapooa au kuolewa.

 

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.