Nafasi za Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Cheti na Stashahada 2014/2015 Hizi Hapa!

Je wewe ni miongoni mwa watu wanaopenda kusomea Ualimu?

Kuanzia mwaka huu wa masomo 2014/15 wanafunzi watakaojiunga na fani ya Ualimu kwa masomo ya Sayansi na Hisabati watagharimiwa na Serikali kupitia mfumo wa ruzuku na mkopo.

166520_373381459424873_1954327802_n

Wanafunzi watakaokuwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza watapatiwa Ruzuku na wale wenye Daraja la Pili na la Tatu watapewa mkopo ili kuwasaidia katika masomo yao. Watakaofaulu mafunzo ya ualimu katika masomo ya Sayansi/Hisabati watapatiwa ajira moja kwa moja kulingana na taratibu za serikali.

Fursa hii ni ya kwako hakikisha unaomba mapema kadri utakavyoweza bila kusahau katika maombi yako zingatia vitu vifuatavyo:

Namna ya kutuma maombi:

a) Waombaji watume maombi yao kwa njia ya MTANDAO (online application) kupitia tovuti zifuatazo: www.moe.go.tz AU www.nacte.go.tz

Maombi kwa njia ya mtandao yataambatana na ada ya shilingi 10,000 itakayolipwa kwa kutumia MPESA. Maelekezo ya kina kuhusu namna ya kutuma maombi kwa njia ya mtandao yanapatikana katika tuvuti ya wizara www.moe.go.tz na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi www.nacte.go.tz

Malipo ya maombi yanaweza kufanyika kupitia MPESA kama ifuatavyo:
1. Piga *150*00#
2. Chagua 4. (Lipa kwa MPESA);
3. Chagua 1. (Weka LIPA Namba);
4. Weka LIPA Namba (ingiza namba 607070);
5. Ingiza kiasi (ingiza kiasi cha 10,000.00);
6. Weka Enter Reference No. ( ingiza 1234);
7. Weka namba ya SIRI (ingiza namba yako ya siri); na
8. Ingiza 1 kuthibibitisha malipo.

AU

b) Barua kwa:

KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)

Source: moe website

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

11 thoughts on “Nafasi za Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Cheti na Stashahada 2014/2015 Hizi Hapa!

  1. ushauli tu si ombi mwanafunzi anapoomba nafasi za masomo apewe nafasi na sio anaomba anaweza ukapita miaka miwili au asichaguliwe kabisa analazimika kukaa nyumbani na kuamua kuolewa au kuoa kutokana na mda mwingi aliopoteza serikali tendeeni kazi ushauli huu.

    Like

  2. Nimejaribu kutumia hii namba ya M Pesa mliyotoa imegoma sasa nifanyeje, na mda ndio hivyo umeenda kweli nifanyeje? naomba mnisaidie . Pili ili suala la Stashahada miaka mitatu kwa ualimu maalumu miaka mitatu kwa wale waliofaulu A, B, na C, kfundisha Secondary nimeipenda sana ila jamani tukiomba tunaomba tupewe nafasi, maana mimi vigezo hivyo ninavyo ila nimeomba mara moja sikuwah kupata sasa nimeomba tena na sijui kama nitapata.

    Like

  3. serikali tunaomba sana ushrikiano wenu, kwel watu tunawito wa fani ya ualimu ila tunaomba kla mwaka hatupati, mfano mimi, basi tunaomba basi hata taarifa kupitia kwa email zetu kwamba mtu hajapata kwa sababu gani! ili tujue sio kusubri penye hakuna jamani!

    Liked by 1 person

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.