Ushairi na Mashairi | Istilahi za maneno!

166520_373381459424873_1954327802_n
Kuna baadhi ya maneno ambayo yamekua yakitumika mara kwa mara katika nyanja ya Ushairi. Hivyo kwa leo tunakuletea baadhi ya istilahi ambazo wewe kama mwalimu tarajali unaweza kukutana nazo katika mitihani yako ya mwezi Mei mwaka huu. Istilahi hizo ni hizi;
 • VINA

Hizi ni silabi za kati na mwanzo katika mshororo

 • MIZANI

Hii ni idadi ya silabi katika mshororo

 • MSHORORO

Huu ni mstari mmoja wa shairi katika ubeti

 • BETI

Hiki ni kiwango cha mishororo iliyo na maana/wazo

 • MWANZO

Huu ni mshororo wa kwanza katika ubeti

 • MLOTO

Huu  ni mshororo wa pili katika ubeti

 • MLEO

Huu ni mshororo wa tatu katika ubeti

 • KIISHIO

Huu ni mshororo wa mwisho usiyojirudiarudia katika beti

 • KIBWAGIZO

Huu ni mshororo wa mwisho unaojirudiarudia katika beti

 • VIPANDE

Hili ni tamko la pumzi moja la mshororo katika urari na muwala wa shairi

 • UKWAPI

Hiki ni kipande cha kwanza cha mshororo

 • UTAO

Hiki ni kipande cha pili cha mshororo

 • MWANDAMO

Hiki ni kipande cha tatu cha mshororo

 • MKINGO

Hiki ni kipande cha mwisho cha mshororo

Karibu katika ulimwengu wa Ushairi.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “Ushairi na Mashairi | Istilahi za maneno!

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.