Jipime Katika Somo la Uraia – II | Septemba 2014

1276785_582156798487698_1688053981_oSEHEMU A

Jibu Maswali yote katika Sehemu hii

 1. Nyumbulisha istilahi zifuatazo kama zinavyotumika katika elimu ya siasa-uchumi;
  • PATU
  • PANA
  • MAYAZI
  • GATT
 2. Kwa kutoa mifano tofautisha vitendo vya Ujifunzaji na Vitendo vya Ufundishaji kama ilivyo katika mtiririko wa ufundishaji somo la Uraia.
 3. Unaelewa nini juu ya Uraia wa Nasaba? Taja sifa tatu (3) za raia mwema wa Tanzania.
 4. Taja Nchi mjumbe (ambaye sio wa kudumu) wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 5. Mabadiliko ya mwaka 2010 ya Katiba ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1984 yanaainisha muundo mpya wa ngazi za uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ainisha ngazi tatu (3) tu za muundo huu mpya.
 6. Bunge la Jamhuri ya Muungano hufanya vikao vyake vinne (4) kwa mwaka. Taja vikao hivyo.
 7. Mada zifuatazo za Uraia hufundishwa katika madarasa gani shule za Msingi?
  • Alama za Shule na za Taifa,
  • Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
  • Katiba ya Tanzania,
  • Sera na mipango ya Uchumi,
 8. Ainisha misingi minne (4) ya mfumo wa uchumi wa kijamaa.
 9. Taja nchi nne (4) za pembe ya Afrika.
 10. Bainisha aina za wabunge ambao si wa kuchaguliwa kutoka katika majimbo ya uchaguzi wanaounda Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la sasa.

SEHEMU B

Jibu Maswali Mawili (2) kutoka Sehemu hii.

11. Fafanua malengo manne(4) ya milleniam.

12. Eleza kwa ufasaha madhumuni yasiyopungua matatu (3) wa ujifunzaji wa somo la Uraia kwa mkurufunzi.

13. Tathimini faida na hasara zisizopungua tano (5) za ushirikiano kati ya Tanzania na Mataifa mengine.

SEHEMU C

Jibu maswali Mawili (2) tu kutoka sehemu hii.

14. Andaa andalio la somo darasa la V juu ya mada kuu: Uongozi wa Serikali za Mitaa, Mada ndogo:Dhana ya serikali za mitaa,malengo mahsusi;kueleza maana ya serikali za mitaa,na kuainisha vyanzo vya mapato katika Serikali za Kata.

15. Fafanua misingi isiyopungua mitano (5) na wala isiyozidi sita(6) ya ufundishaji wa somo la uraia kwa shule za msingi.

16. Pendekeza mapendekezo manne (4) ambayo Tume ya Taifa ya Katiba unafikiri ingeweza kuyaweka katika mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya ya Tanzania.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “Jipime Katika Somo la Uraia – II | Septemba 2014

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.