Jipime Katika Somo la Uraia – I | Septemba 2014

1404865_595576347145743_1610672151_o

Sehemu A

Jibu Maswali yote katika Sehemu hii.

 1. Taja nchi nne za pembe ya Afrika
 2. Mchakato wa uundwaji wa Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ilipitia hatua mbalimbali. zitaje hatua hizo za kikatiba.
 3. Nyumbulisha istilahi zifuatazo kama zinavyotumika katika somo la uraia;
  1. WTO
  2. BAKITA
  3. SAP
  4. FGM
 4. Taja vyama nane (8) vya siasa vilivyo na usajili wa kudumu isipokuwa CCM,CUF,CHADEMA,NCCR-MAGEUZI na TLP.
 5. Taja sababu nne (4) zilizopelekea Tanganyika na Zanzibar kuungana mwaka 1964.
 6. Taja sikukuu nne (4) za Kitaifa ambazo si za kidini na tarehe zake.
 7. Taja aina mbili za mashauri ya mashitaka ya mahakama unayoyafahamu.
 8. Uingereza ni miongoni wa nchi zinazotumia katiba mapokeo. Taja vitabu vinne (4) tu vinavyounda katiba ya nchi hiyo.
 9. Taja vipengele vinne (4) tu vinavyounda Katiba ya Tanzania.
 10. Taja mambo muhimu manne (4) muhimu ambayo ni ya muungano.

Sehemu B

Jibu Maswali Mawili (2) tu

11. Taja na eleza kwa mifano madaraka na mamlaka aliyonayo Rais wa Tanzania juu ya Bunge la Tanzania.

12. Fafanua mfumo rasmi wa Mahakama hapa Tanzania

13. Vyama vya upinzani vinakazi kubwa Bungeni. Fafanua kazi zisizopungua tano (5).

Sehemu C

Jibu Maswali Mawili (2)  tu

14. Fafanua viashiria sita (6) vya utandawazi vya kitamaduni.

15. Migogoro katika bara la Afrika imekuwa Dondandugu. Jadili.

16. Unafikiri ni sababu zipi zilizosababisha matokeo ya kidato cha nne mwaka huu hususani katika shule za umma maarufu kama shule za kata kuwa mabaya?

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

3 thoughts on “Jipime Katika Somo la Uraia – I | Septemba 2014

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.