- Taja na fafanua kwa kifupi stadi mbili za lugha za muhimu kwa mtoto ayeanza kujifunzia lugha.
- Bainisha misingi minne kati ya misingi ya hati nzuri.
- Toa maelezo kwa kifupi kuhusiana na istilahi zifuatazo:
- Tathilitha
- Takhmisa
- Tarbia
- Tathnia
- (a) Utungaji ni nini?
(b) Taja aina kuu mbili za utungaji.
- Tunga sentensi nne kuonesha maana tofauti za neno ‘paa’.
- Huku ukitumia mifano, toa tofauti kati ya kauli ya ktendea na kauli ya kutendewa.
- Toa maelezo mafupi kuhusu dhana zifuatazo:
- Fonimu
- konsonanti
- sarufi
- semantiki
- Kwa kutumia neno ‘vizuri’, tunga sentensi mbili ukionesha kivumishi cha sifa na kama kielezi
- Taja na kufafanua matawi manne ya sarufi
- Toa maana ya istilahi zifuatazo:
- azimio la kazi
- kiongozi cha mwalimu
- Shajala ya somo la Kiswahili
- Nukuu za somo
SEHEMU B (ALAMA 30)
11. Orodhesha mambo muhimu yanayopaswa kuonekana katika barua rasmi kisha toa mfano wa kuandika barua rasmi fupi ya kuomba kazi ya ukarani kwa mkuu wa wilaya. Tumia anuani yoyote.
12. Somo la Fasihi halifundishwi katika shule za msingi. Kanusha au kubali hoja hii kwa hoja madhubuti.
13. (a) Taja aina tano za kauli za utendaji na kwa kila aina ya kauli tunga sentensi moja.
(b) Bainisha aina ya maneno yanojenga senteni zifuatazo:
- Baba anasoma kitabu na mama anaandika barua
- kijana mrefu alifungua dirisha mwanafunzi hodari amefauru mtihaani wake vizuri
- Mwalimu mwema amemsaidia mwanafunzi wake
- Wanafunzi wawili wanacheza mpira mkubwa na mwalimu wao anaandika barua fupi
14. Jadili mambo ambayo husababisha mtoto ashindwe kusoma.
SEHEMU C (ALAMA 30)
15. Eleza mambo muhimu ambayo utazingatia wakati unamfundisha mwanafunzi wako utungaji wa shairi la kimapokeo
16. Kwa kutumia mifano, fafanua dhana na sifa za viazishio vya somo.
17. Unafikiri mbinu zuri ya kufundishia somo la Kiswahili ni ipi?
18. “ Kutumia zana za kufundishia na kujifunzia ni kupoteza muda’’ . Jadili
Nimefurahia maswali yenu mbalimbali pamoja na mitihani,napenda kupata notes za English,mitaala,ushauri na unasihi pamoja na somo la ICT. Mwalimu tarjali kutoka Mandaka T.c
LikeLike
nimeyaelewa maswali nahitaji mengi zaidi
LikeLike
asante kwa maswali mazuri
LikeLike
askante mwl gunda kazi nzuri kutoka tabora tc
LikeLike
nimependa
LikeLike
nisaidieni maswal yafuatayo:
1.maana ya mtaala
2.sifa za mtaala
3.umuhimu wa mtaala
4.aina za mitahala
LikeLike
1 MITAALA NI JUMLA YA MAMBO YOTE YALIYO RATIBIWA KUFUNDISHWA KATIKA SHULE ZA MISINGI, UPILI NA VYUO. (AINA ZA MTAALA A,MTAALA RASMI B,MTAALA FICHO C,MTAALA USIO RASMI) SIFA ZA MTAALA ! UZINGATIE KIWANGO CHA WALENGWA/WANAFUNZI
LikeLike
Stadi kuu za lugha za muhimu ni STADI ZA KUZUNGUMZA NA STADI ZA KUSIKILIZA
LikeLike
Nilikuwa naomba msaaada wa maswali na majibu ktk somo la uraia niweze kujua baaadhi ya maswali mangumu
LikeLike