UFUGAJI WA SAMAKI KATIKA MAZINGIRA YA KIJIJINI KWA MTAJI MDOGO

1

Na: Meshack Maganga – Iringa. Go Big or Go Home

Ndugu zangu, juzi Ijumaa nilikuwa kwenye maongezi ya kawaida na Dada yangu, mwalimu na mshauri wangu Dada SUBIRA, ambae ndiye mmiliki wa Blogu ya WAVUTI. Tulikuwa kwenye maongezi ya kifamilia, kisha nikamshirikisha harakati zangu za ufugaji wa samaki, akapata hamasa, akaniomba niwashirikishe na Watanzania wenzangu kwa maandishi. Na mimi nikakubaliana na ombi hilo.

Unaweza kufanikiwa sana tu, unaweza kuwa billionaire ama milionea. Chunguza marafiki zako na watu unaoshinda nao waliofanikiwa, jifunze kwao na usipojifunza utaendelea kuwa mlalamikaji.Fursa ya ufugaji wa samaki, kilimo cha miti, kilimo cha nyanya na vitunguu ishakudondokea, usijjite myonyenge, ama maskini maana ‘victim mentality isn’t going to get you anywhere’ GO BIG OR GO HOME.

Ninachokiamini katika maisha yangu ni kwamba, kila mtanzania anayonafasi kubwa sana ya kuendesha maisha yake ya kila siku bila tatizo endapo atajitambua na kuugundua ukuu wa Mungu ndani yake. Mwanadamu yeyote anaetambua uthamani wake na bahati aliyopewa na Mungu ya kuendelea kuishi na kuzaliwa Tanzania hawezi kuishi maisha ya kubangaiza.

b

Katika Makala yangu ya wiki hii ningependa kuwashirikisha kitu kidogo sana nacho ni UFUGAJI WA SAMAKI KATIKA MAZINGIRA YA KIJIJINI KWA MTAJI MDOGO SANA… kipindi cha nyuma, nilikuwa nikiwaona watanzania wenzangu hasa huku Iringa, wakijishughulisha na ufugaji wa samaki, ni miaka miwili imepita sasa, lakini nilikuwa ‘bize’ na mambo yangu sikutaka kujifunza Zaidi kuhusu fursa hii. Mwanzoni mwa mwezi wa nane (8) mwaka jana 2014 rafiki yangu Nicolaus Kulangwa, ambae huko nyuma alinifundisha kilimo cha Matango,alinipigia simu akinitaka nikataembelee mradi wake wa kufuga samaki. Nilienda kijini kalenga hapa Iringa. Nilichokiona nilianza kukifanyia kazi hapohapo na siku ileile. Wakati rafiki yangu akiwa na jumla ya mabwawa saba ya samaki aiana ya sato na pelege mimi ndio kwanza nilijutia muda ambao niliambiwa kuhusu fursa ile halafu nikazembea kuifanya.

Kama tunavyofahamu, lengo la uajasirimali ni kupata faida ya unachokifanya na kugusa jamii inayo mzunguka mjasirimali. Na kama ilivyo kwa mifugo mingine yeyote ile, kabla ya kuanza kufuga kuna mambo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa ili ufugaji wako uweze kuwa tija iliyokusudiwa na hivyo kufikia malengo ya mfugaji huyo. Lakini kutokana na mazingira ya ufugaji wa huku Iringa hasa Kalenga, nitayataja mambo hayo kwa kifupi sana, mambo haya huenda yakatofautiana kutoka eneo moja la nchi hadi jingine, na kwa vile mimi sijasomea chuo cha ufugaji wa samaki, maelezo haya ni yale niliyoyapata kwa uzoefu tu, siyo ya kufundishwa chuo, mapungufu yatakayogundulika na ‘wasomi’ wataniandikia email ili nikawashirikishe wenzangu.

Mambo hayo ni kama ifuatavyo:

 • ENEO AMA SEHEMU YA KUWAFUGIA SAMAKI. Inasisitizwa kwamba, eneo hilo liwe na udongo mzuri ambao hautaruhusu maji kupotea hovyo. Udongo wa mfinyanzi ni mzuri na iwapo eneo lako lina udongo wa tifutifu ama udongo wake ni kichanga unashauriwa kujengea kwa simenti ama kuweka ‘kapeti gumu’ lisilo ruhusu maji kupotea.
 • UPATIKANAJI WA MAJI, wote tunafahamu kwamba samaki huiishi majini, maji ndiyo roho ya masaki, samaki ni maji na maji ni samaki. Hivyo eneo la kufugia lazima liwe na maji ya kutoshana salama kwa kipindi cha mwaka mzima. Vyanzo vya maji kwa ajili ya ufugaji wa samaki ni kama chemichemi, mito, maziwa na maji ya ardhini hasa visima Kwa maeneo ya huku Iringa, tunabahati ya kuwa na mto Ruaha ambao maji yake yapo muda wote wa kipindi chote cha mwaka. Inashauriwa kwamba eneo hilo liwe salama ili kuwalinda samaki na mfugaji kwa ujumla.
 • BWAWA. Bwawa la samaki linahitaji nafasi kubwa ya ardhi, yenye mwinuko pamoja na eneo la samaki kukimbilia. Hii ni njia rahisi ya ufugaji endapo ardhi na maji havina gharama kubwa. Eneo kubwa zaidi linaruhusu uzalishaji usiohitaji nguvu ya ziada na wenye tija.
 • MBEGU AMA VIFARANGA, mfugaji wa samaki anashauriwa kutembelea maeneo ambayo wafugaji wakubwa wanazalisha vifaranga ili aweze kupata mbegu bora anayohitaji. Kwa wananaoishi Iringa na maeneo ya jirani, wanaweza kupata mbegu kwa bwana Nicolaus.
 • UTUNZAJI WA BWAWA NA USAFI. Ili mfugaji aweze kunufaika na miradi ya kufuga samaki ni lazima uafanye usafi wa kutosha ndani nan je ya bwawa lake. Hasa kwa kuondoa majani ili kuepusha wadudu na viumbe wengine kama konokono,vyura, nyoka, na kenge wasiweze kufanya makazi na hatimaye wakawadhuru samaki. Hivyo, kila unapoona uchafu, safisha mara moja.
 • ULISHAJI. Tofauti na mifugo mingine kama kuku, samaki hawahitaji kula chakula kingi sana. Katika hatua za mwanzo ulishaji wake unaweza kuwa mara tatu kwa wiki ama Zaidi.
 • AINA YA CHAKULA. Samaki wanaweza kulishwa kwa kutumia pumba ya mahindi, mashudu ya pamba na alizeti, soya, mabaki ya dagaa, Karanga zilizosagwa, unga wa mahindi, mabaki ya chakula kama ugali nk.
 • Kuna mambo mengi sana ya kuzingatia unapaanza kufuga samaki, mambo mengine ni kama vile kuzingatia miiundo mbinu, wafanyakazi, kuzingatia masoko, utaalamu nk.
 • CHANGAMOTO KATIKA SAMAKI ni magonjwa kama vile magonjwa ya samaki yapo mengi yakiwa nayasababishwa na vimelea vifuatavyo magonjwa yanayosababishwa na bakteria, magonjwa yanayosababishwa na virusi magonjwa yanayosababishwa na minyoo, magonjwa yanayosababishwa na protozoa. na magonjwa yanayotokana na lishe duni. Chanagamoto nyingine ni kama vile, Tatizo mojawapo ni la kuvuja kwa kuta za bwawa. Tatizo hili hutokea iwapo ujengaji wa bwawa haukufuata maagizo na taratibu za ujengaji wa bwawa. Kuna ndege, kenge, fisi maji, nyoka hutokea. Iwapo bwawa lipo mbali na makazi. Kudumaa kwa samaki kutokana na kuwa wengi bwawani kupita idadi inayotakiwa.
 • UVUNAJI WA SAMAKI. Hujudi za mfugaji ndio zinaweza kupelekea kuvuna samaki wa kutosha na kumletea faida kwa muda mfupi. Wakati wa kufaa kuvuna samaki bwawani hutegemea ukuaji na aina ya samaki. Ukuaji wa samaki pia hutegemea ubora wa chakula. Samaki wanaofugwa katika bwawa lenye hali nzuri watakuwa tayari kuvunwa baada ya miezi 6 hadi 8. Kuna watakao sema huu ni muda mrefu, ukiona ufugaji wa samaki wanatumia muda jaribu kingine. Ama endelea kukaa nyumbani kwako, ukiisubiri serikali na mashirika ya kijamii yakusaidie.

iku

Nielezee kwa kifupi jinsi ufugaji wa samaki unavyochangia ajira binafsi kwa watanzania na faida yake kwa ujumla. Changamoto mbalimbali za kiuchumi, na ukosefu wa ajira kwa wasomi wanaotoka vyuo vikuu kwa sasa, imesababisha watanzania wengi kuanza kuwa wabunifu na kuanza kujishughulisha na ujasiriamali hasa kilimo na ufugaji. Kwa sasa mabwawa mengi yanapatikana katika mikoa sita yenye rasilimali nyingi kama Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Mbeya na Ruvuma. Ufugaji wa samaki umeenea kote nchini.

Kwa sasa kilo moja ya samaki huuzwa shilingi 7,000/ kwa huku Iringa na ukiuuzia bwawani kwa jumla ni shilingi 4000/ kwa kilo. Hii ina maana kwamba ukiwa na kilo mia 7 za samaki una uhakika wa kuwa na milioni mbili na laki nane kila baada ya miezi sita, kama utauzia bwawani kwa bei ya shilingi elfu 4 kwa kilo ambapo hii ni samaki watatu tu aina ya sato, je ukiwa na samaki ama kilo elfu tano? Utagundua kwamba adui wa mafanikio yako ni sentensi za kizamani ulizo weka kichwani kwako.

d

Niseme wazi tu kwamba, ufugaji wa samaki, ni fursa nyingine ambayo ipo wazi kwa kila Mtanzania kuifanya, kuna watakao singizia mitaji, hali ya hewa nk,lakini ukweli ni kwamba bwawalangu dogo nilitumia pesa ndogo sana kulichimba ikiwa ni pamoja kununua vifaranga vya samaki.

Tumekuwa watu wa kujiwekea mipaka ya mafanikio vichwani mwetu. Kumbuka kwamba ukishajiwekea mipaka ya mafaniko. Maisha yetu yataweza kubadilika iwapo tutabadilisha namna tunavyoyatazama mambo. Kwa mfano unaweza kuwa umejiwekea mipaka ya kimapato kwamba wewe mwisho wako ni kupata laki moja, mtazamo huo ukikaa kichwani basi ukiambiwa bwawa moja linaweza kukutolea shilingi milioni 25 kwa miezi sita, utakataa na hivyo fursa hiyo itakupita.

Nilipokuwa nikisoma kitabu cha ‘THE TRUTH SHALL MAKE YOU RICH’ cha reallionaire mdogo kuliko wote Farrah Gray kwa sasa, nimejifunza kwamba, maisha yetu yanaweza kubadilika muda wowote na dakika yoyote iwapo tutajijengea Imani kwamba, maisha yanawezekana popote. Na kwa Tanzania hii ambapo kila mwananchi anaruhusiwa kulimiliki ardhi kwenye mkoa wowote umasikini litakuwa ni swala la kujitakia.

Ninamalizia makala hii kwa kusema kwamba, kila saa katika maisha yetu ni fursa, makala hii pia ni fursa kwako na kwangu, kuna baadhi ya nchi duniani ambapo wananchi wake hawana bahati ya kukaa kwenye meza zao na kujifunza mambo haya. Kwawatakao penda kuja Iringa, kujifunza ufugaji wa samaki, tunawakaribisha sana. Nicolaus na mimi na wafugaji wengine watakusaidia kuapata elimu Zaidi yahii niliyoandika hapa.

e

“MY MOTTO IS GO BIG OR GO HOME”
Binadamu wote wenye mafanikio duniani hawachoki kutafuta..!
MAWASILIANO:
meshackmaganga@gmail.com
facebook.com/pages/Fresh-Farms-Trading

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

51 thoughts on “UFUGAJI WA SAMAKI KATIKA MAZINGIRA YA KIJIJINI KWA MTAJI MDOGO

 1. Ahsante sana ndugu kwa elimu hii nzuri. je iwapo sina sehemu ya kuchimba bwawa ninaweza kujenga tank la nzege ndani ya chumba? nikutakie mafanikio mema katika kutuzibua masikio ya fursa zilizopo.

  Liked by 1 person

  1. inatakiwa kwanza kujua unataka kufuga samaki wengi kiasi gani ila cha msingi ni hewa na mwanga wa kutosha kwa samaki na maji yawe yanauwezo wa kubadilishwa mara kwa mara ila ukichimba bwawa ni bora zaidi

   Like

 2. Asante ndugu kwa makala hii,kimsingi nimetamani kufuga samaki,swali langu,je naweza kufuga samaki katika simtank lile kubwa kabisa?

  Like

  1. Unaweza Leila ila cha msingi hakikisha wasiwe wengi zaidi pia hakikisha wanakua na uwezo wa kupata hewa na mwanga wa kutosha na uhakikishe inakua rahisi kubadilisha maji yao kwa wepesi bila kuwadhuru

   Like

   1. watanzania bana, hebu weka mambo wazi ivi unaposema ulitumia pesa kidogo kuchimba bwawa na kununua mbegu ni kiasi gani? eleza mchakato wewe sio unaandika tu masentesi yako ya kukaririshwa kuchimba bwawa ni shi ngapi mbegu shi ngapi kuwalisha chakula shi ngapi mpaka wanakuwa tayari nyambafu

    Like

 3. NDUGU MESHACK ASANTE SANA KWA ELIMU HII YA UFUGAJI WA SAMAKI, MIMI NIMEANZA KUCHIMBA BWAWA NITAOMBA NIKUSUMBUE NITAKAPO HITAJI MSAADA TOKA KWAKO,KWANI UMEONGEA MAMBO MAZITO YA KUJIKWAMUA NA UMASKINI.

  Liked by 1 person

 4. Jamani mimi natamani kufuga samaki wa maji baridi hasa SATO, lakini wengi wanaojitangaza kama wataalam wa ufugaji wa SATO wamekuwa wasanii kama wanasiasa wa Tanzania. Cha ajabu ni kwamba hata wasomi, viongozi waliopewa dhamana katika kuendeleza ufugajji wa samaki wamekuwa hawasemi kweli kama si wanasema uongo. Kwa mfano kuna watu wengi wamekuwa walimu akijigamba kwamba wanafahamu ufugaji wa samaki na wengine wanasema wanafuga wenyewe na miezi sita tu SATO anakuwa na uzito wa gram 800 hadi gram 1000. Kwa kweli nimewatembelea wengi ukweli wa mambo ni kwamba wote niliowatembelea pamoja na kuwa walijigamba na wengine kupitia katika vyombo vya habari ni kwamba samaki wao wako kati ya gram 80 hadi 300 tu. Hivi ni kwa nini watanzania tumekuwa wongo hivi?

  Like

  1. Kiufupi kama samaki utamfuga namna inavyohitajika kwa kutumia mbegu safi na maji pia kuwa hata na vipimo vyo maji kwa nafasi pana ama bwawa lenye manzari nzuri zaida samaki hukua vizuri kufikia 1kg kwa miezi 6 ila wengi wao hukosa elimu kiundani juu ya suala la ufugaji wa samaki hivyo matokeo samaki hudumaa kutokana na sababu za kielimu na si kwamba wataalam wa ufugaji wa samaki wanasiasa ndugu kuwa mpole tafadhali.

   Like

 5. Asante, Ninaomba unisaidie kujua ukubwa wa eneo/shamba ambalo mtu anaweza kufugia samaki, ili nianze kulisaka nami niweze kuanza ufugaji wa samaki (hebu jaribu kuniba eneo la mabwawa mawili, baraba yahani nafasi kati ya bwawa na bwawa ili nijue kiasi cha ardhi nitakacho hitaji).

  Liked by 1 person

  1. Eneo la kufugia samaki inategemeana na wewe unahitaji bwawa uweke samaki wangapi ila kadri bwawa linavyokua kubwa ndivyo samaki wako watakua na uhuru zaidi wa kupata chakula na uzalianaji utakua mzuri.

   Wiki hii tutajaribu kuweka vipimo vya kila namna kwa kila bwawa ili ujue kwa kina

   Like

 6. ASANTE KWA ELIM YAKO. MI NIKO MUSOMA NAOMBA KUJUA UREFU WA BWAWA KWENDA CHN PIA VIFARANGA SI RAHISI KUPATA KWA KUNUNUA NA NIKO KARIBU NA ZIWA. JE KUNA UWEZEKANO WOWOTE WA KUCHUKUWA HATA SAMAKI WAKUBWA ILI WAZALIANE?

  Like

  1. UWEZEKANO WA KUCHUKUA SAMAKI WAKUBWA UPO ILA INATEGEMEANA NA AINA YA SAMAKI UNAETAKA KUMFUGA NDUGU YANGU. KWA MAELEZO ZAIDI 0658530884.

   Like

 7. Asante Sana kwa elimu hii, labda swali langu ni vipimo sahihi vya bwawa, meta ngapi kwenda chini najua urefu itategemea na idadi ya samaki. Kazi njema

  Like

 8. mita moja ya mraba huweza kuishi kambale wangapi? na je bei ya vifaranga vya kambale ni sh. ngapi kwa kutosha bwawa la ukubwa wa mita 15 urefu na 6 upana. navipataje nipo shinyanga

  Like

 9. Asante ..kaka nakupa big up sana kwani unachokisema ni cha kweli. ila kwa anae hitaji kufuga samaki anapaswa kuzingatia ushauri kutoka kwa wataalam wa ufugaji wa samaki.

  Like

 10. Asante Meshack kwa ushauri wako wa ufugaji samaki mimi niko Kagera na nimeanza kuchimba bwawa la samaki ila nitahitaji ushauri wako juu ya ufugaji .hongera kwa elimu unayotoa kwetu .

  Like

 11. Ninashukuru sana kwa elimu hii ya ujasiriamali, mimi naomba msaada kuhusu maandalizi ya eneo la kuchimbia bwawa, jinsi ya kusakafia, kiwango cha maji katika bwawa lenye kina cha mita 1.5, na maji yanapaswa kubadilishwa baada ya muda gani? na Utajuaje kama samaki wanaumwa? au kuna chanjo? je, inafaa kutumia maji ya mvua yaliyovunwa?
  Ninawapongeza sana kwa elimu hii muhimu sana.

  Like

  1. nashukuru kwa ushauri wako Mimi binafsi nimependa mradi huu wa ufugaji wa Samaki nilitaka kujua vipimo vya mabwawa ili nianze na uchimbaji wa bwawa kitalam upana urefu na kina chini na kiasi gani Samaki wanaweza kukaa na ningependa kufuga Samaki wadogo wadogo ambao hata mtu wa chini ananudu kuwanunua naomba msaada wako mpendwa nipo mbozi vwawa

   Like

  1. samaki 1000 wanahitaji eneo la mita za mraba 125 ambayo ni sawa na mita 10 kwa 12.5
   Kwa ufugaji wa kawaida mita moja ya mraba inahitaji samaki 8 lakini kama una utunzaji na ubadilishaji wa maji mara kwa mara, mita moja ya mraba inachukua samaki 10.

   Like

 12. Ufugaji bora wa samaki ni dawa bora kabisa na tiba sahihi ya ugonjwa wa maisha. Chagua kuwa unavyotaka kuwa kivitendo; ishi njozii yako, ifanyie kazi kupitia ufugaji wa samaki.

  Like

 13. Nashukuru kwa elimu yako juu ya samaki lakini naomba nijue changamoto zingine mbali na hizo za bacteria na kuvuja kwa kingo je vipikuhusu maji yanayoingia bwawani endapo yanatoka sehemu za viwandani yanaweza kuwa na madhara kwa samaki?

  Like

 14. Ahsante kwa somo nzuri.
  ukipitia mawazo ya watu wengi walitoa comments kuna mambo machache ambayo yanahitaji ufafanuzi kutokana na uzoefu wako.
  1.Ukubwa wa bwawa na idadi ya samaki katika bwawa. Nina maana urefu x upana x kina na idadi ya samaki.
  2. Magonjwa ya samaki na tiba zake.
  3. Upatikanaji wa vifaranga bora (wengi wanouza vifanga wanasema wana vifaranga vizuri lakini ni wababaisha na unakuwa huna uwezo wa kuhakikisha kama wanachosema ni sahihi) Kuna njia ya kufuhamu vifaranga bora naomba ushauri).
  4. Maji yanapaswa kubadirishwa baada ya muda gani, na unatoa maji yote au yanabakia kiasi fulani?
  5. Kiwango cha chakula kulingana na idadi ya samaki kina kinakuwaje. Nina maana kama samaki 1000 wantakiwa kula kilo ngapi kwa siku na unawapa mara ngapi kwa siku.
  6. Unahitaji watu wangapi kuhudumia samaki 2000.
  7.Naomba nipate mchanganuo wa chakula (ratio ya virutubisho sahihi ili kupata mchanganyiko sahihi ili kuepuka vyakula vya kununua ambavyo wakati mwingine vinakuwa si sahihi)
  Ahsante nitakutafuta kwa simu.
  Naitwa
  Abdi Dar es salaam

  Like

 15. Asante sana kwa elimu nzuri ya ufugaji wa samaki .Nimeingia kuperuz hapa baada ya kila siku ninawaza ninamnagani samaki anafugwa.
  Naomba elimu zaidi uchimbaji wa mabwawa yani kina na ukubwa wa bwawa

  Like

 16. asante mkuu kwa elimu ya ufugaji samaki please naomba kufahamu gharama za utengenezaji wa bwawa moja kubwa litakaloweza kubeba samaki 1500

  Like

 17. pia naitaji kujua maeneo mahususi ya ufugaji wa samaki je Dodoma unaweza kufuga samaki kutoka na hali ya hewa .naomba kufahamu hayo mkuu

  Like

 18. Mkuu nimefurahia makala yako, imenipa uelekeo mpya juu ya ufugaji. binafsi nilijikita katika ufugaji wa kuku lakini sasa naona ni wakati muafaka kupanua wigo wangu kwa kuanza ufugaji wa samaki. Nitakutafuta muda punde nikianza mchakato. Lazima kieleweke.I don’t want to go home I want to go big as your motto “GO BIG OR GO HOME” is concerned.

  Like

 19. somo nimelipenda tena sana, mwenye sikio amesikia, mwenye kusoma katambua! (mtu hasifiwi kwa mipanga, bali husifiwa kwa kutekeleza mipango) tume fumbuliwa macho, mwenye kutaka kuona na aone, mwenyekutaka kuendelea kufumba macho, aendelee. maana ndo maisha kachagua, MESHACK! KEEP IT UP”

  Like

 20. somo nimelipenda tena sana, mwenye sikio amesikia, mwenye kusoma katambua! (mtu hasifiwi kwa mipanga, bali husifiwa kwa kutekeleza mipango) tume fumbuliwa macho, mwenye kutaka kuona na aone, mwenyekutaka kuendelea kufumba macho, aendelee. maana ndo maisha kachagua, MESHACK! KEEP IT UP”

  Like

 21. Thx for the good advice, nimependa na imenivutia sana,ila naomba kuuliza,Je,maji ya samaki yanatakiwa kubadiliahwa baada ya muda gani,tangu kuwekwa kwa samaki?

  Like

 22. Hello,Thanks for share this great and interesting article with us, this topic is really important for help people to improve your health problems bringing efficient solutions and tips. wow I am impressed, keep up the good work.Best rebedrs,Sagastian |

  Like

 23. Une vente légale de cannabis entrainera inévitablement un marché parallèle moins cher car certains revendeurs souhaiteront rester dans l’ombre et seront prêts à baisser leurs tarifs…Pourtant, cela devrait être fait si les sommes récoltées servent à la prévention, aux soins des personnes dépendantes et à la lutte contre tous les réseaux mafieux….Le Tonton Flingueur

  Like

 24. Comment’s author: velella01/02/07 08:24:00 AMDear Gene, long time no see~~<br />你還真是一點都沒變,其實你只是懶而已吧?<br />有趣的是從本篇第三張照片看來,<br />你的書架上最顯眼的一本書是 Wine,<br />再來是 Sex,然後才是 DNA,<br />這有什麼科學上的解釋嗎?XD<br />Happy New Year!<br /><br />PS. 加油!早點畢業我也許有機會當你的學生….

  Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.