Rubani wa Kwanza Mwanamke Nchini Ghana – Patricia Mawuli Nyekodzi

gg

Patricia ni rubani wa kimisheni, injinia wa ndege, mwelimishaji wa mekanika wa rotax na Teknolojia ya Anga.
Patricia anatokea Ghana, nchi iliyoko Afrika Magharibi. Takribani miaka 4 iliyopita Patricia alitokea kijijini na kwenda kutafuta kazi.

Alifanya kazi ya kung’oa visiki na kungo’olea majani kwenye barabara ya kurukia kwa urefu wa mita 1000 kila wiki, aliifanya kazi hiyo kwa mikono. Hivi sasa, Patricia amekuwa mhamasishaji mashuleni na katika sehemu za kazi nchini Ghana; na pia ni injinia wa ndege, rubani na mwalimu wa kurusha ndege. Umri wake ni miaka 23 tu.


Patricia anaona mafanikio yake yamejijenga kwenye UPENDO. Anapenda sana ndege, anaipenda nchi yake, na anawapenda watu wake. Aidha, ni mwanachama hai wa Medicine on the Move ( Utabibu wa masafa) ambapo anapenda kuokoa maisha kila arukapo.


Patricia angependa kushirikisha historia ya maisha na mafanikio yake; jinsi alivyofaulu kutoka maisha duni ya kuishi kwenye kijumba cha udongo kijijini hadi kuwa mtengeneza ndege na mwendesha ndege katika nchi yake ya asili; hadi kujulikana kama mwanamke kijana wa mfano kote Afrika Magharibi.

“Vijana yawapasa kuelewa kuwa kufanyakazi kwa bidii ndiyo siri pekee ya mafanikio na ni lazima uzingatie kile ukifanyacho kama unataka kufanikiwa kimaisha.” – Patricia Mawuli Nyekodzi.

www.njiampya.com

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.