Dr. Reginald Mengi Atoa Shindano la Biashara la 3N (‘Nitabuni wazo la biashara, Nitatekeleza, na Nitafanikiwa’)

mengi-main2

Maelezo kuhusu shindano

Shindano

Shindano la Wazo la Biashara kwa kifupi 3N, ikiwa ni kifupisho cha ‘Nitabuni wazo la biashara, Nitatekeleza, na Nitafanikiwa’ kufanyika kuanzia Januari 8, 2015 hadi Juni 30, 2015

Malengo

 • Dk Reginald Mengi ana lengo la kutoa changamoto kwa wajasiriamali kufikiria mambo makubwa mapya yanayohusu biashara.
 • Shindano hili limeandaliwa kwa lengo la kushawishi wajasiriamali wa Tanzania kuyafanyia kazi mawazo yao na kuibuka na biashara zenye tija.
 • Shindano hili litamtoa mshindi mmoja kila mwezi ambaye anayetaka kubadili wazo kuwa biashara kwa ruzuku ya sh milioni 10 ili kulifanyia kazi wazo lake la biashara kwa kulitekeleza kwa vitendo.

Masharti

 • Shindano linawashirikisha Watanzania pekee
 • Shindano linaendeshwa kwa njia ya mtandao wa Twitter ambapo mshiriki atatuma wazo lake la biashara kwa anuani ya twita @regmengi
 • Dk Mengi atatumia timu ya washauri elekezi kuweza kumpata mshindi wa kila mwezi, na maamuzi hayo yatakuwa ya mwisho.
 • Katika mchujo wa kwanza jopo la washauri elekezi litateua mawazo bora zaidi na kuingia katika mchujo wa pili ambapo watapewa kiunganishi ili waweze kujaza fomu ya kutoa maelezo zaidi.
 • Watu kumi (10) waliotoa mchanganuo nzuri watafanyiwa usaili kwa njia ya simu ili jopo hilo lijiridhishe kama maelezo waliyotoa wakati wanajaza fomu ni yao binafsi, na kama wamejipanga vizuri kutekeleza kibiashara.
 • Kutokana na mawazo hayo 10 teule, jopo litachagua wazo moja kuwa mshindi.

Maswali yanayoulizwa kila mara kuhusu Shindano la wazo la Biashara la 3N

Swali: Ni njia gani mtu anaweza kushiriki katika shindano
Jibu: Njia pekee ya kushiriki ni kwa kutuma wazo lako kupitia mtandao wa twitter tuu kwenda @regmengi

Swali: Kwa nini shindano hili linaendeshwa kupitia mtandao wa twitter?
Jibu: Nia ya shindano hili ni kuhamasisha matumizi bora ya mitandao ya kijamii.  Dr Mengi ameamua kuanza na twitter kama njia rahisi anayotumia kwa mawasiliano.

Swali: Ni mawazo mangapi mtu anaweza kutuma?
Jibu: Mshiriki anaruhusiwa kutuma mawazo mengi kadri inavyowezekana.

Swali: Kwa nini unaweka wazi wazo lako?
Jibu: Ni kuzidi kuchochea ubunifu. Wengine wakiona wazo lako linawasukuma kuliboresha. Na wewe ukiona wazo lako limeboreshwa unapata changamoto ya kuliboresha zaidi ili ushinde. Hivyo mawazo yanakuwa bunifu zaidi.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

6 thoughts on “Dr. Reginald Mengi Atoa Shindano la Biashara la 3N (‘Nitabuni wazo la biashara, Nitatekeleza, na Nitafanikiwa’)

 1. wazo langu la biashara endapo nitafanikiwa kuwa mshindi Wa kwanza Wa 3n kuna sehemu nyingi sana zina matatizo ya maji nitachimba tenk la chini lenye ujazo Wa Lita laki moja nitajenga banda la bati lefu mita 100 mgongo Wa tembo litakuwa na gatazi ambazo mvua ikinyesha inaingiza maji kwenye tenk msimu mzima Wa mvua nitawauzia maji wananchi kwa bei nzuri ya t sh 200 kwa Lita 20 endapo tenk litajaa kwa Lita laki moja nitapata milioni20 pia nitakuwa nimepunguza japo kidogo shida ya maji wananchi mladi huu nategemea kuufanya kwenye maeneo yenye shida ya maji kama kijiji cha msijute na hiyari maji kule ndoo moja mia tano mpaka mia saba maji menyewe niya chumvi nitawasaidia wengine ili wapate maji ya kunywa yasio na chumv I hilo ndilo wazo langu kubwa la biashara

  Like

 2. wazo jingine la tatu nikifanikiwa kuchaguliwa 3N nitafanya hivi kuna mashirika ya nyumba yanajenga nyum
  ba na kuziuza kwa wananchi kwa bei nafuu ukweli ni kwamba mashirika haya yapo mjini Tu Mimi nitafanya hivi nikifanikiwa nitaingia kijijini nitaonana na viongozi Wa kijiji nitajenga nyumba mbili zenye samani ndogo sana isiozidi milioni NNE kila moja nitauza kwa njia ya mnada sitalenga masilahi makubwa sana ili niuze kwa haraka na kuendelea kujenga zingine kuna wafugaji wengi wakulima hawajui matumizi ya pesa pesa inatakiwa ikutunze cio uitunze mawazo yangu tote haya yanalenga vijijini najua ndio kwenye matatizo makubwa hilo ndilo wazo langu la tatu namtanguliza mungu ktk mawazo yangu yote

  Like

 3. alex Thom’s

  Alex thomas Nipo geita mkoa mpya Tel 0759341386 wazo langu la biashara kuhusu kilimo cha miti nikibahatika kuchaguliwa 3N ya Dk Mengi nitatimiza ndoto yangu yakumiliki kampuni Nitaanzisha kilimo cha miti ya mbao laini (seplas) hekari tati niche elfu tatu ya kisasa mpaka kufikia mavuno ni miaka kumi natano hapo ndipo kampuni yangu itakapo anza wakati huo mti mmoja utakuwa na thamani ya laki mbili mpaka tatu (mti 1unaweza toa mbao 20to 30) nitanunua misumeno ya injin nitaajiri watu kufanya kazi hiyo wakati huo nikikata mti napanda mti kuendelea kulinda mazingila nakuendeleza kampuni yangu huu ni mladi mkubwa niwachache ambao wanaweza kuutekereza .Mradi huu nimkubwa sana nainawezekana tens vizuri sana kwa mtu mwenye nia kama wazo hili kwangu nilasiku nyingi mwaka Wa tano sasa lipo kichwani sibahatishi .Naimani wazo langu litaeleweka kikubwa tumwombe Mungu

  Like

 4. Wazo langu la Biashara ni linahusu mboga za majani kama mchicha nk’ kwa asilimia 98 hadi 100 watu wengi wanatumia mboGa za majani,hata kiafya mboga za majani ni muhimili ,,mkubwa na tunashauliwa kila mlo tuwe na mboGa za majani,mboga za majani zinawateja wengi sana,historia inaonyesha wengi tunafanya biashara hizi katika mazingira ambayo si salama kwa mlaji na mlaji pia hapati ubora wa kile wanachonunua kwani kuna mazingira ya uchafu,vumbi na atimaye kupoteza viini lishe vilivyomo kwenye mboga,kitu kipya ninachotaka kufanya katika dunia hii ya utandawazi ni ubora wa bidhaa kwa afya ya walaji kwa hiyo basi mimi nimeipenda biashara hii kutoka moyoni kwa sababu 1.ghalama ya kuanzisha biashara hii yaani capital ni ndogo 2.walaji ni wengi,ubunifu wangu binafsi ni huu hapa ni kusambaza mboga hizi kwa kutumia toyo au pikipiki ya taili tatu nita sambaza mboga kwa umbali zaidi bila kuchoka tofauti na sasa,kuuza mboga kwa kuweka kwenye madeli meupe yakiwa ndani ya pikipiki madeli haya yatafanya mboga zionekane vizuri,vijana wenzangu watapata ajira na tatizo la ajira kwa eneo langu kwa asilimia chache litpungua,mjini nimeona min na super market nyingi lkn sijaona inayouza mboga za majani kwa wingi ila mimi nitakuwa wa kwanza,maono yangu kama mjasiliamali mdogo niwe na ofisi kubwa inayojishughurisha na mboga mboga tu,ghalama za mboga hizi kama sina eneo la kulima nikijumua fungu ni 300 moja mara fungu 2000 sawa na 600000mtaji,bei ya kuuza fungu moja ni 500 mara 2000 sawa na 1000000 kwa siku faida 400000 mara mwezi 30 sawa na 12000000 kwa mwaka ni 12 sawa na 144000000 fedha hii itaongeza mashamba na ajira, inawezekana, 0689448662

  Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.