Kauli 10 CHAFU za Walimu Darasani | Jiandae Vema Kwenda BTP!

Katika wiki mbili hizi zilizopita tumekua na maandalizi ya kwenda kufanya mazoezi ya ufundishaji (BTP) vyuoni mwetu. Yapo mambo mengi ambayo Wakufunzi wametuasa na kutusisitiza muweze kukamilisha zoezi zima la kozi yako ya Ualimu na uweze kuhitimu ukiwa Mwalimu Bora.

Kwa ujumla Haiba ya Mwalimu ndio msingi mkuu unaokuongoza na kukutambulisha mbele ya Wanafunzi wako na Walimu wenzako.

10533852_302712236576870_1789663602341715221_nMuda mrefu walimu wengi wamekua wakijisahau wanapokua darasani na kutoa kauli ambazo kwa namna moja ama nyingine zinawaathiri watoto (wanafunzi).

Ni vema Mwalimu akajitahidi kujizuia na hisia binafsi hata kama mtoto atakua hakuelewi; upendo na kutambua kazi yako kama mwalimu ndio mafanikio ya mwanafunzi wako; wapende jaribu kuwasaidia kadiri ya uwezo wako.

Hizi ni baadhi ya Kauli 10 CHAFU za walimu darasani, ni vema kujiepusha na maneno kama haya darasani ukiwa kama mwalimu;

1: Mkimaliza kuongea niambieni niendelee kufundisha
2: Baba yako kauza ng’ombe ili alete ng’ombe mwingine shule
3: Kama unajua kuliko mimi njoo ufundishe wewe
4: Ulikuja peke yako na utaondoka peke yako
5: Hata msiponisikiliza mshahara wangu uko pale pale
6: Baba yako anahangaika kulipa ada wewe unafanya utumbo tu
7: Hata nikeshe nafundisha wengine ni mizigo hawatoki na lolote
8: Tunavisaidia tu kwan vikifanikiwa mbelen hata salam vinatoa?
9: Bichwa kubwa ubongo nukta
10: Wengine hapa wamekuja kukua tu

Tunawatakia mazoezi mema ya Kufundisha.

Mwalimu Gunda

2

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

5 thoughts on “Kauli 10 CHAFU za Walimu Darasani | Jiandae Vema Kwenda BTP!

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.