Jipime na Mtihani wa Stadi za Kazi | Sehemu ya Kwanza

10394774_1488170148116726_2329008715773573721_n1. Bainisha sifa nne za rangi ya maji.

 1. (a) Orodhesha vifaa vitano vinavyotumika katika usukaji wa ukili kwa njia moja.

(b) Eleza kwa kifupi namna ya kuchana ukindu.

 1. Taja mambo manne ya kuzingatia wakati wa kughani shairi.
 2. Bainisha mbinu nne za uimbaji.

 3. (a) Eleza stadi ya udobi ni nini?

(b) Katika mazingira ya chuo chako ,watu hutumia vifaa gani kwa ajili ya kufulia nguo? Taja vifaa vitano.

 1. Ainisha mbinu nne utakazotumia katika ufundishaji wa mada ndogo ya upambaji wa nguo kwa mafundo.
 • Taja kanuni nne za usalama wa mpishi.

 • Eleza kwa ufupi maana ya:

 • (a) Kitabu cha mwalimu.(b) Kiongozi cha mwalimu.

  1. Toa sabababu nne za mwalimu wa stadi za kazi kuwa na nukuu za somo.
 • Nini maana ya Andalio la somo?

 • SEHEMU B (Alama30)

  Jibu maswali mawili (2) kutoka katika sehemu hii.

  1. Taja aina tano ya mishono unayoweza kushona kwa mikono na eleza matumizi ya kila mshono.
 • Katika ufugaji bora wa kuku wa kienyeji hakuna haja ya kuwatunza kuwa kienyeji kwani wanauwezo mkubwa wa kujitafutia chakula chao ” Jadili usemi huu.

 • Eleza kazi za sehemu za kamera zifuatazo,

 • (i) Kasha (ii) Kiangalizi (iii) Apecha (iv) Swichi ya shata (v) Kisogezafilamu (vi) Kirekebishi cha fokasi

  (vii) Lenzi    (viii) Shata   (ix) Kimweko.

  1. Kwa nini tunajifunza kuhusu biashara ndogo ndogo, hali ya kuwa sisi ni walimu? Kwa nini tusijifunze kuhusu Maazimio na Maandalio pekee?

  SEHEMU C (Alama 30)

  Jibu maswali mawili (2)kutoka katika sehemu hii.

  1. Katika ufundishaji wa somo la stadi za kazi vitendo huchukua nafasi kubwa. Eleza umuhimu wa kutumia zana za kufundishia na kujifunzia kwa mwanafunzi.
  2. Fafanu au muhimu wa Muhtasari wa somo la stadi za kazi.

  3. Wewe kama mwalimu wa somo la Stadi za kazi, Azimio la Kazi lina umuhimu gani katika ufundishaji?

  4. Eleza manufaa ya upimaji kwa mwalimu wa somo la stadi za kazi.

   

  Jiunge na Kundi la WhatsApp la “Walimu na Ualimu” ili uweze pata majibu ya Maswali haya hapo juu au jiunganishe kupitia Namba hii: 0683400780

  Author: Sir Gunda

  A Friend of Education

  2 thoughts on “Jipime na Mtihani wa Stadi za Kazi | Sehemu ya Kwanza

  Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

  Fill in your details below or click an icon to log in:

  WordPress.com Logo

  You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

  Google photo

  You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

  Twitter picture

  You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

  Facebook photo

  You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

  Connecting to %s

  This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.