Ualimu kama Kazi ya Kitaalamu | NECTA 2012

hEleza kwa ufasaha sababu tano (5) zinazofanya ualimu uwe kazi ya kitaalamu (NECTA 2012).

  1. Utaalamu hutoa huduma kwa jamii – mwalimu kama mtaalamu hutoa huduma kwa wanafunzi anaowafundisha na kwa jamii kwa ujumla. Mwalimu hutoa huduma ya maarifa na ujuzi mbalimbali kiasi kwamba bila mwalimu usambazaji wa maarifa na ujuzi kwa jamii ungetumia muda mrefu. Mwalimu pia hufundisha wanafunzi maadili mema, na mwenendo bora ili aweze kukubalika katika jamii anamoishi.
  2. Una miiko ya kazi – Utaalamu una miiko ya kazi ambayo hueleza kinaganaga uhusiano kati ya mtaalamu na mteja wake ambayo inamlinda mteja. Katika Tanzania Tume ya Utumishi wa Walimu inaeleza miiko katika kazi ya walimu na pia Chama cha Walimu kinasisitiza kimsingi udumishaji wa miiko ya walimu kazini.
  3. Una utaratibu unaofahamika wa kumwendeleza mfanyakazi – kila kazi ina namna yake ya kutoa mafunzo kazini. Katika ualimu kumekuwa na mafunzo ya aina mbalimbali ya kumwendeleza mwalimu.
  4. Una utaratibu mahsusi wa mawasiliano – kuanzia ngazi ya chini kabisa mwalimu anautaratibu mahsusi wa mawasiliano kuanzia kwa mwalimu mkuu hadi waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi.
  5. Huduma kwanza kabla ya mapato – kazi ya ualimu mara nyingi imeweka mbele suala la huduma kuliko kipato, vipato vinavyotolewa kwa walimu mahali pengi ni vidogo ikilinganishwa na huduma inayotolewa na walimu hao.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “Ualimu kama Kazi ya Kitaalamu | NECTA 2012

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.