Mambo matano (5) ya Kuzingatia wakati wa Matayarisho ya Ufundishaji | Msingi Mkuu wa Mwalimu

Matayarisho ya Ufundishaji ni nini?

DSC06283Haya ni maandalizi anayoyafanya mwalimu kabla hajaanza kuingia darasani kufundisha somo alilopangiwa au analokusudia kufundisha.

Jambo la kwanza katika kufanya maandalizi ya ufundishaji ni kuchambua muhtasari wa somo na vitabu vya kiada kwa somo husika ili kubaini mada kuu na mada ndogo zilizopo na kuzipangilia kimantiki kufuatana na mazingira ya ufundishaji unaoukusudia. Uchambuzi wa vitabu husaidia kurekebisha makosa au kubadili kumbukumbu kuendana na wakati, hasa kwa dhana ambazo hubadilika mara kwa mara.

Jambo la pili ni kusoma rejea au makala mbalimbali zinazohusu mada unayotarajia kufundisha ili kujua nini cha kuandaa; mfano zana, majaribio au ziara n.k. Kusoma pia husaidia kuongeza uelewa juu ya mada unayotarajia kufundisha na masuala mtambuka.

Jambo la tatu ni kubainisha mada zenye maudhui yanayofanana katika muhtasari wako na masomo mengine ili kuwashirikisha walimu.

Jambo la nne ni uandaaji wa azimio la kazi

Jambo la tano ni uandaaji wa somo (andalio la somo) na zana pamoja na mbinu za kufundishia.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

5 thoughts on “Mambo matano (5) ya Kuzingatia wakati wa Matayarisho ya Ufundishaji | Msingi Mkuu wa Mwalimu

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.