MAWAZO YA WANAFALSAFA JUU YA ELIMU YA AWALI | FRIEDRICH FROEBEL

2

Froebel anashika nafasi ya pekee kati ya wataalamu wa mambo ya malezi. Ijapokuwa mawazo yake makuu yalifanana na yale ambayo ROSSEAU alikuwa amekwisha kuyaandika.

Alizaliwa ujerumani mwaka 1782 katika kijiji kilichokuwa katika msitu wa Turingia.Akiwa kijana bado alifanya kazi chini ya uangalizi wa Bwana misitu,na kwa nafasi hiyo alijipatia moyo wa kupenda uoto wa asili juu ya sura ya nchi,na pia kupenda maumbile ya asili ya nchi.

Baadaye alijiunga na chuo kikuu cha Jena ambapo kaka yake alikuwa pia akisoma.hapo aliendeleza ujuzi wake wa mambo ya sayansi na hisabati.Ulimwengu mzima ulilazimika kumsikiliza Froebel kwa makini kwa sababu kuu mbili

  1. Kwanza Froebel alikuwa mwalimu maarufu sana ambaye alijenga shule yake mwenyewe na katika shule hiyo akatekeleza kwa matendo yale aliyo kuwa ameyanena kwa maandishi.
  2. Pili matokeo ya mafanikio ya shule hiyo yaliwatia moto wafuasi wake,nao wakayachukua mawazo ya mwalimu wao kwa moyo wa kitume,wakayaeneza katika sehemu mbalimbali za dunia,liliundwa hata shirika la kimataifa la kueneza mawazo ya froebe,shirika ambalo lilisaidiwa na kuungwa mkono na matajiri wengi.

Sifa kuu ya Froebel imo hasa katika kuzua wazo la kuwa na shule za Chekechea (kindergarten)jina hili la Kindergarten ambalo lina maana ya “bustani ya watoto”  ndilo hasa lililoeleza imani na msimamo wa Froebel juu ya malezi.Yeye alimlinganisha mtoto na mmea mchanga,na kazi ya mwalimu akailinganisha na kazi ya mkulima bustani,ambaye wajibu wake ni kutengeneza mazingira yanayofaa illi mmea ukue wenyewe hata kufikia kikomo chake.

Mawazo yake kuhusiana na elimu na jinsi ya kumuandaa mtoto kielimu ni haya yafuatayo:

Froebel alipendekeza pawe na umoja katika mambo yanayofundishwa na kutaka tuepuke hatari ya kuyagawa masomo katika sehemu ndogondogo zisizohusiana kwa mfano yeye alihimiza kuwa mitaala ya masomo ionyeshe umoja.Aliwalaumu pia waalimu wa vyuo vikuu ambao walikuwa wameligawa somo la malezi katika sehemu nyingi ili waandike vitabu.

Alisema pia katika shughuli ya malezi uhuru wa mtoto ni muhimu kuzingatiwe , “ sisi binadamu tunapotunza mimea na wanyama tunawaachia nafasi ya kujimudu na pia muda wa kukua,tikijua kuwa kwa kufanya hivyo mimea yetu na wanyama wetu watakuwa sawa sawa kdili ya asili ya kukua: tunawapa fursa ya kupumzika na hatuyaingilii maisha yao kinguvunguvu,wala hutuwafanyi vitendo vyovyote vitavyozuia kukua kwao.

Lakini mtoto wa binadamu tunamfanya kama kipande cha nta au donge la udongo ambalo tunaweza kuligeuza kuwa umbo lolote tulitakalo,kwa nini hatutaki kujifunza kutokana na jinsi mama dunia anavyokuza viumbe vyake!
Katika hili pia alisema kazi ya mlezi/mwalimu ni kumfuata na kumlinda mtoto,isiwe kazi ya kumwamuru,kumkatia mashauri au kuyaingilia maisha yake.

Jambo lingine Froebel anafikiri kuwa ni muhimu kwa kila mlezi kuhakikisha kwamba mahitaji ya mtoto ya akili, vionjo na mwili yanatimilizwa katika kila kipindi cha kukua kwake. Ili maendeleo ya mtoto yaweze kutimilika katika kipindi fulani cha kukua ni lazima maendeleo ya kipindi kilichotangulia yawe yametimilika kwanza,ni lazima mwalimu afahamu vizuri tabia na mahitaji ya watoto katika kila kipindi cha kukua kwao.

Froebel pia alitlilia mkazo vitendo kuliko nadharia vitu vya kuchezea kuliko vitabu,stadi za mikono kuliko stadi za akili mawazo yake yalifanana na yale ya ROSSEAU katika hili,lakini pia Froebel alitilia mkazo ujengaji wa uhusiano mwema kati ya watoto jambo ambalo ROSSEAU hakutilia maanani.

Jambo lingine kubwa katika Mawazo ya Froebel linaoandamana na mawazo yake juu ya kukua kwa watoto,ni kucheza,anasema kuwa kucheza ni njia pekee inayokuza uwezo wa watoto kujifunza.Anasema
“kucheza ndilo jambo bora kabisa katika maendeleo ya mtoto,kucheza ni kujieleza kwa mawazo na vionjo ambako hutokana na msukumo wa mtoto ulio ndani ya mtoto.Hii ndio maana ya neno kucheza”

Anaendelea kusema kwamba katika kucheza mtoto hukuza vipawa vitakavyojionyesha zaidi katika utu uzima,mtoto achezapo hujenga misingi ya tabia yake ya baadaye iwapo atakuwa mtu mpole au mkatili,mkarimu au mwenye choyo,mvivu au mwenye bidii,mpumbavu au mwerevu,mharibifu au mtunzaji vitu.

Pia Froebel anazungumzia jambo alilotilia mkazo ROSSEAU yaani ubora wa kumshughulisha mtoto wakati anapojifunza(shughuli ya mtoto mwenyewe).Alionyesha pia faida ya uongozi wa mwalimu,na faida ya mtoto kujifunza pamoja katika vikundi vidogovidogo,au pengine kujifunza pamoja wakiwa darasa zima,alipendekeza pawe na uwiano wa kufaa kati ya kumwacha mtoto  kujishughulisha peke yake,na kuongozwa na mwalimu,na pia kati ya kumwacha mtoto ajifunze peke yake na kumshirikisha na wenzake.

Kwa kweli madhumuni ya njia za kujifunzia alizopendekeza Froebel yalikuwa kuwapa watoto uzoefu wa kweli wa kisayansi,kwa kuanzia na upekuzi wa mambo yaliyowapendeza watoto wenyewe.Mafunzo juu ya maumbile ya asili,kama vile sura ya nchi,mimea na wanyama yalipewa nafasi kubwa katika ratiba ya masomo,na mara nyingi masomo yalifanywa nje ya darasa ili watoto waweze kuyaelewa mazingira yao.

Ijapokuwa Froebel alikazia jambo hilo la kujifunza kwa vitendo alionya pia kwamba katika kufanya vitendo vya aina mbalimbali watoto wasilazimishwe kushindana kwani si jambo zuri kumlinganisha mtoto mmoja na watoto wengine.,badala yake kila mtoto ashindane na yeye mwenyewe yaani kila mara ajaribu kufanya vizuri kuliko alivyofanya mwanzo.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

2 thoughts on “MAWAZO YA WANAFALSAFA JUU YA ELIMU YA AWALI | FRIEDRICH FROEBEL

  1. Hongera Frobel kwa ufafanuzi juuya ujifunzaji Wa watoto na nimeelewa kitu kipya kuwa ni vizuri mtoto ajifunze zaidi kwa vitendo ili kujua vitu katika mazingira yake kwa kutumia vitendo zaidi kuliko nadharia.

    Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.