MAWAZO YA WANAFALSAFA JUU YA ELIMU YA AWALI | JEAN JACQUES ROSSEAU (1712-1778)

JEAN JACQUES ROSSEAU (1712 – 1778)

10478233_10155150705010401_2660249828977346818_n

Alizaliwa mwaka 1712 katika mji wa Geneva huko Uswisi ambako alipata mafunzo yake ya awali kutoka kwa baba yake na baadae kutoka kwa mkufunzi aliye kuwa ameajiliwa kumfundisha.Kitabu Emili ndicho hasa kilichoeleza mawazo yake juu ya malezi ya watoto.

ROSSEAU alikuwa na mwelekeo wa kuamini kuwa kwa asili watoto huzaliwa na tabia nzuri na kwamba mazingira  huwafanya wawe na tabia mbaya.Alisisitiza njia bora ya kuwaelimisha  watoto ni kuwaweka katika hali ya asili ambayo itamwezesha kukuza tabia,silika zao za uwezo wao bila kuathiriwa na mazingira

Aligawanya maisha ya mtoto katika hatua nne

  1. Hatua ya kwanza ni ya utoto mchanga, huu ni wakati mtoto anapojenga mazoea na tabia njema ni wakati unao faa kumwongoza mtoto kutawala maono yake
  2. Hatua ya pili ni mtoto mdogo, huu ni wakati wa kujifunza namna ya kutumia milango yake ya maarifa
  3. Hatua ya tatu ni mwanzo wa uvulana au usichana hiki ni kipindi cha akili mtoto anapotumia akili yake juu ya vitendo anavyofanya
  4. Kipindi cha nne ni uvulana au usichana mpevu (baada ya miaka 15) hiki ni kipindi cha fikra za kiroho,hapo mtoto anatambua hasa mema na mabaya

ROSSEAU alieleza umuhimu wa mtoto kuwa kitovu cha elimu ili kumpa hali nzuri ya maisha.Alisisitiza kuwa elimu lazima imsaidie mtoto huyo kuwa huru na mwenye furaha,elimu imsaidie mtoto kukuza haiba nzuri ili elimu iweze kufikia malengo haya lazima itolewe kufuatana na hali na hatua za kukua kwa mtoto.

Mtoto afundishwe jinsi ya kujifunza na jinsi ya kutatua matatizo katika mazingira malimbali,Alisisitiza kuwa elimu ni haki ya watoto wote ni chombo kinachoweza kuyatawala mazingira ya mtoto.

Alishauri kuwa ufundishaji  uende sambamba na hatua za ukuaji wa mtoto.uzingatie upevu na utayari wa mtoto katika kujifunza.

Njia bora za kufundishia ni zile zinazomsaidia mtoto kutumia milango mingi ya fahamu inavyowezekana ili kufanikiwa katika jambo hili mwalimu atumie zana za kufundishia hasa kwa kutumia vitu halisi.
Katika ufundishaji mwalimu atumie njia zitakazo mwezesha mwanafunzi kujifunza kwa vitendo.
Ili watoto wawezekujifunza kwa urahisi mwalimu aanze kufundisha mambo yanayofahamika kuelekea mambo yasiyofahamika.

Falsafa ya ROSSEAU  juu ya elimu inafanana na falsafa ya elimu Tanzania .
Rosseau alikazia kuwa mitaala na ufundishaji imlenge mwanafunzi yaani mwanafunzi awe msingi wa  kuzingatiwa katika elimu,kwenye kujitegemea jambo ambalo limesistizwa pia kwa mfano elimu ya kila ngazi inasisitizwa ijitosheleze yaani mwanafunzi amalizapo ngazi moja ya elimu aweze kujitegemea.

Kufuatana na Rosseau elimu lazima izingatie mahitaji ya maadili,katika falsafa ya elimu ya kujitegemea ufundishaji wa maadili umezingatiwa kwa kuwafundisha wanafunzi masomo ya siasa na dini.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

2 thoughts on “MAWAZO YA WANAFALSAFA JUU YA ELIMU YA AWALI | JEAN JACQUES ROSSEAU (1712-1778)

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.