John Dewey alizaliwa mwaka 1859 huko Vermont,Marekani na alifariki mwaka 1952 akiwa na umri wa miaka 93.Dewey aliandika mengi na kufanya mengi yaliyo mfanya atambuliwe na dunia kuwa mwamba katika utaalamu wa falsafa na pia kuwa mwlimu hodali na mtu aliye kuza nadharia inayohusu malezi ya watoto.
Kutokana na kazi ya Dewey zilianzishwa shule zilijulikana kama shule za maendeleo, na malezi yaliyo tolewa yakaitwa malezi ya maendeleo,akiwa Michigan Dewey alianzisha kituo cha watoto wadogo alichokiita shule ya maabara mwaka 1896 alikusudia shule hiyo itoe nafasi ya kufanya utafiti na majaribio juu ya namna ya kujifunza.
Dewey alisisitiza kuwa elimu haiwezi kutengwa na jamii kwa hali hiyo basi, elimu ni njia ambayo jamii huitumia katika kulinda kuendeleza na kuhifadhi utamaduni wake.Madhumuni ya elimu basi ni kutayarisha na kutoa raia walio bora na wanaoweza kuitumikia jamii yao kikamilifu.
Dewey aliamini kuwa katika kutenda au kufanya shughuli fulani wanafunzi wanaweza kuelewa mambo vizuri zaidi.Alisisitiza kuwa maarifa hupatikana kutokana na shughuli wazifanyazo watoto.
Kuhusu suala la kujifunza Dewey alitaja mambo ambayo ni muhimu kuzingatia wakati wa kumfundisha mtoto.Mambo hayo ni haya yafuatayo
- Mwanafunzi mwenyewe lazima awe katika mazingira halisi ya aina ya uzoefu anaotakiwa kupata
- Lazima kuweko na tatizo la kweli linaloamsha na kuchochea mawazo na ari ya mwanafunzi ya kutatua matatizo.
- Mwanafunzi mwenyewe lazima afanye uchunguzi na atafute au akusanye data za kumsaidia katika kulitatua tatizo lake.
- Ni lazima ajaribu kutafuta ufumbuzi mbalimbali wa tatizo hilo.
- Ni lazima apate muda wa kufanya majaribio kuona kama mawazo au dhanio alizozipata ni kweli zinaweza kuwa na uthibitsho wowote
Dewey alilisisitiza kuwa shule iwe kaya njema ambamo mtoto atafundishwa maadili yote ya jumuiya yake,shule iwe kaya njema ambamo mtoto atafundishwa maadili yote ya jumuia yake shule imjenge mtoto kimwili kiakili na kitabia.
Dewey hakuona umuhimu wa mgawanyo wa mafunzo katika masomo kama ilivyo hivi sasa kwa mfano,historia, Jiografia,hisabati,na sayansi bali alihimiza kuwa masomo yote yatolewayo hapana budi yazingatie
- Shughuli anazofanya mtoto mwenywe
- Shauku aliyo nayo mtoto wakati wa kujifunza
- Matatizo anayopambana nayo
- Mahitaji yake ya kila siku
Nashukuru nukuu ziko vzr
LikeLike
pia isemekane kuwa mtoto ni zao la jamii,sio la familia pekee,Bali pia jamii pia jamii inao wajibu mkubwa wa kumufunza mtoto katika nyanja zote za makuzi na malezi ya mtoto .ni Mimi,Silas Francis,kutoka chuo cha ualimu kabanga(diploma ya elimu awli)0757237726.
LikeLike