MAWAZO YA WANAFALSAFA JUU YA ELIMU YA AWALI | MARIA MONTESSORI (1870- 1952)

MARIA MONTESSORI (1870- 1952)

66

Alizaliwa Italia alikuwa mwanamke wa kwanza nchini Italia kuwa daktari wa magonjwa ya watoto na magonjwa ya akili.Katika ugunduzi wake alingundua kuwa watoto waliovia akili wanaweza kufunzwa kwa kutumia vifaa vya kuchezea wanavyovipenda.Aliamini kuwa tatizo la kuvia akili ni la kielimu na sio la tiba.

Montessori aliamini kuwa elimu ya mtoto ni lazima ianze mapema sana kwa sababu umri wa mtoto  kati ya kuzaliwa  hadi miaka sita ni muhimu sana kwa ujenzi wa haiba yake.

Ili mtoto aweze kujifunza kwa ufanisi zaidi ni muhimu kwa mzazi au mwalimu kutumia michezo na vitendo vinginevyo katika kufundisha,hii itamsaidia mtoto katika kujifunza kujifunzia stadi mbalimbali za utendaji .

Pia alipendekeza mwalimu atumie vifaa vingi katika ufundishaji,vifaa hivyo viwe ni vile vinavyokuza tabia ya udadisi na ugunduzi,vinavyompa nafasi ya utendaji na vinavyomwezesha kufanya majarabio,kutatua vikwazo,ujasiri,kuuliza na kujibu maswali,kupenda kufaulu, kujiendeleza na kumpa msukumo wa kujitegemea katika utendaji.

Alitaka watoto wenyewe wajishughulishe kikamilifu katika kila kitu wanachofanya katika mazingira yaliyo tayarishwa  vizuri na mwalimu kwa kuwapatia  vifaa muhimu vinavyo hitajiwa.

Alibuni michezo ya kujifunzia,alitumia vifaa vya kuchunguza ambavyo humpatia mtoto maarifa  na hapo hapo kukuza stadi wakati anapovichezea.Alifanya kazi ya kujifunza iwe ni rahisi na ya kufurahisha kwa kutumia vifaa vya kuchezea,vifaa hivyo vya kujifunzia vinaweza kutengenezwa kwa mti, vipande vya nguo,chuma,au karatasi nene.

Kuhusu vyumba/nyumba za madarasa ya watoto alipndekeza igawanywe katika vyumba vingi na kila chumba kiwe kwa ajili ya kufanyia shughuli maalumu tofauti, watoto wawe huru kutembea na kuingia kila chumba  wakitakacho bila kizuizi.

Wanafunzi wajifunze kwa kushirikiana na hali inayotakiwa mle vyumbani iwe ya kuheshimu haki na kazi za kila mtu.Watoto wadogo wajifunze kutoka kwa wenzao walio wakubwa.,vifaa vilivyomo katika nyumba kwa mfano viti vya kukalia viwe vidogo kama walivyo watoto wenyewe.

MARIA MONTESSORI   anajulikana sana kwa kuwa mtu aliyeanzisha njia ya kuwafundisha watoto wadogo.Njia yake ya kufundishia watoto wadogo aliigawa katika sehemu kuu zifuatazo

  1. Elimu inayohusu ukuzaji wa stadi mbalimbali za misuri ya watoto,elimu hii ni nzuri kwa kumsaidia mtoto aweze kukuza stadi zake na kufikia upeo wa juu katika kutumia viungo vyake vya mwili,ili kufikia hali hii wanafunzi wafanye mazoezi mbalimbali ya kutembea na kupumua.mazoezi haya humfanya mtoto awe na umbo zuri na pi humsaidia kujenga mazoea ya kutumia lugha vizuri. Pia alitumia elimu ya aina hii ya mazoezi yanayohusiana na maisha ya kila siku ya mtoto kwa mfano usafi wa mwili,usafi wa mazingira ya ndani na ya nje.
  2. Elimu inayohusu ukuzaji wa milango ya fahamu, mazoezi aliyoyapendekeza kwa watoto ni yale ya kuwasaidia watoto kuweza kutofautisha  kati ya uwingi na ubora wa kitu,mazoezi yanayotumiwa  katika elimu hii ni yale ya kuona na kusikia.
  3. Elimu inayohusu weledi,mazoezi ya kuwapa wanafunzi ni yale ya kumtayarisha mtoto kusoma kuandika na kuhesabu kwa mfano mtoto huanza kugusa, kuangalia,kuandika na hatimaye kusoma .Vifaa ni vya lazima sana kwa kukuza elimu ya aina hii,vifaa hivyo ni kama vile shanga za rangi mbalimbali, vizibo vya chupa,vipande vya miti vilivyoandikwa namba,alfabeti zinazoweza kusogezwa au mbegu za mimea,

Kutokana na ufundishaji wake wa watoto wadogo MARIA MONTESSORI  alipendekeza na kusisitiza mambo muhimu yafuatayo

  • Watoto wafundishwe kwa njia ya michezo
  • Watoto wapewe fursa ya kuchagua michezo na hata vifaa vya kuchezea
  • Watoto wapatiwe fursa ya kuwa huru

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.