TAMKO LA HAKIELIMU | HALI YA RUZUKU KWA WANAFUNZI KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

TAMKO LA HAKIELIMU  

10930067_571818096282561_3761350164147276924_n

Kwa mujibu wa mipango ya maendeleo za shule ya msingi na sekondari (MMEM na MMES), shule zinapaswa kupata ruzuku kwa ajili ya kuziwezesha kujiendesha. Shule za msingi zinapaswa kupata ruzuku ya sh 10,000 kwa mwanafunzi, na kwa shule za sekondari ni sh 25,000 kwa mwanafunzi.

Jumla ya fedha inayopaswa kupelekwa shuleni hutegemeana na idadi ya wanafunzi wa shule husika. Ruzuku (capitation) inalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa kununua vifaa, gharama za mitihani, ukarabati mdogo na kununua vitabu.

 HakiElimu imefanya ufuatiliaji wa hali ya ruzuku ya mwanafunzi katika wilaya 10 nchini; Kilosa, Kilwa, Arusha vijijini, Iramba, Bariadi, Ukerewe, Serengeti, Kigoma Vijijini, Manispaa ya Tabora. Jumla ya shule 40 za msingi na 40 za sekondari zilihusishwa.

Hali ya Ruzuku ya Mwanafunzi

Katika robo tatu za mwaka wa fedha 2014/2015 iliyoishia March 31, 2015 wastani wa sh 865 kwa shule za msingi kati ya sh 10,000 ndiyo ilikuwa imepokelewa shuleni kwa shule zilizohusishwa katika ufuatiliaji. Hii inamaanisha kuwa kwa robo tatu za mwaka wa fedha serikali imeweza kutoa asilimia 9 tu ya sh 10,000.

Kwa shule za sekondari changamoto ya fedha za ruzuku bado ni kubwa, hadi kufikia mwezi Machi 2015, shule zimepokea sh 5,516(asilimia 22) ya ruzuku kwa kila mwanafunzi badala ya sh 25,000.

Mwaka 2013/2014 serikali iliweza kutoa tsh 4,200 ya sh 10,000 kwa shule za msingi na sh 12,000 ya sh 25,000 kwa shule za sekondari kwa kila mwanafunzi.

Kwa wastani imebaki miezi miwili tu mwaka wa fedha 2014/2015 kukamilika na muda si mrefu bunge la bajeti litaanza, hivyo kuna kila dalili kuwa ruzuku kwa mwanafunzi itapungua maradufu kwa mwaka wa fedha 2014/2015 hii bado ni changamoto kwa BRN kutekeleza hili kwa kipindi cha miezi miwili iliyobaki. BRN ilidhamiria kuhakikisha shule zinapata ruzuku ya asilimia 100 ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Moja ya changamoto za ruzuku ya mwanafunzi ni uchelewaji wa fedha kufika shuleni ambapo huchukua miezi miwili hadi mitatu kufika shuleni. Mfumo wa BRN ulibaini hili na kuadhimia kuwa fedha za ruzuku kwa mwanafunzi zipelekwe moja kwa moja kwenye akaunti ya shule toka Hazina kuanzia mwaka wa fedha 2014/2015. HakiElimu imebaini kuwa shule zote 80 zilihohushishwa katika ufuatiliaji wa ruzuku zilipokea fedha za ruzuku kutoka Halmashauri badala ya Hazina tofauti na maadhimio ya BRN.

Hii pia ni changamoto, na zinabaki kuwa ni matamko yasiyokuwa na utekelezaji wa BRN na hivyo fedha zitaendelea kuchelewa kufika shuleni na kuathiri ununuzi wa mahitaji ya shule na kutatua changamoto za mazingira ya kufundishia na kujifunzia. 

Tamati

Imebaki miezi miwili kumaliza mwaka wa fedha 2014/2015, Serikali ipeleke fedha kamili za ruzuku kwa shule za msingi na sekondari. Kitengo cha Utekelezaji wa BNR cha ofisi ya Rais kisimamie ahadi ya fedha za Ruzuku kupelekwa moja kwa moja kwenye akaunti ya shule ili kupunguza uchelewaji wa ruzuku kufika shuleni.

HakiElimu bado haielewi kwa nini suala hili limeshindwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2014/2015 ilihali tayari BRN ilishabaini changamoto na kukubaliana na Wizara ya fedha, Wizara ya Elimu na TAMISEMI kuwa fedha zitapelekwa moja kwa moja kwenye akaunti ya shule. 

Viwango vya ruzuku ya wanafunzi kwa shule za msingi na sekondari ni vya zamani na havijabadilishwa muda mrefu ingawa gharama za maisha zimepanda. Serikali ibadilishe viwango hivi kulingana na gharama halisi za sasa.  

 

Kaimu Mkurugenzi

Boniventure Godfrey

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.