Tunawapongeza Shirika la HakiElimu Kupata Mkurugenzi Mtendaji Mpya

Mhe. John Kalage - Mkurugenzi Mpya HakiElimu
Mhe. John Kalage – Mkurugenzi Mpya HakiElimu

 

Bodi ya Wakurugenzi wa shirika la HakiElimu imemteua John Kalage kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa shirika hilo.

John ambaye kitaaluma ni mchumi amechukua nafasi hiyo kuanzia tarehe 1 Mei 2015 kutoka kwa Elizabeth Missokia.

John anakuja na weledi na uzoefu wa zaidi ya miaka 20 ya kufanya kazi kama msimamizi mwandamizi katika mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ya kimataifa katika nchi mbalimbali kama vile Tanzania,Ubelgiji, Afrika Kusini na Zambia.

Aidha, ana uzoefu mkubwa wa usimamizi wa kimkakati; rasilimali fedha na watu; kubuni na kusimamia miradi ya mamilioni ya dola. Katika kipindi chote hicho, John umeonyesha uwezo mkubwa katika utetezi na ushiriki wa sera, kujenga na kuimarisha uwezo wa mashirika ikiwa ni pamoja na asasi za kiraia na kijamii (NGO na CBOs), mashirika ya kitaalamu pamoja na vyombo na taasisi za serikali.

Kabla ya kujiunga na HakiElimu, John alikuwa akifanya kazi katika shirika la kimataifa la Save the Children akiwa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Miradi, jukumu ambalo amekuwa akilitekeleza kwa kipindi cha miaka sita iliyopita. Bila shaka atakuwa anakumbukwa sana katika shirika la Save the Children kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha shughuli za shirika hilo nchini na hususani kwa kulisaidia kufanikisha kupata miradi mbalimbali ya mamilioni ya dola kutoka kwa wafadhili.

Nafasi nyingine ambazo John amewahi kushika ni pamoja na kuwa Mkurugenzi Mkazi wa shirika la kimataifa la Student Partnership World Wide (SPW) nchini Zambia alikofanya kazi kuanzia Aprili 2007 hadi Machi 2009.

John ni Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa mashirika kadhaa, yakiwemo Railway Children Africa na Tanzania Aids Forum. Pia aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania inayoratibu na kusimamia shughuli za Mfuko wa Dunia unaotoa fedha za kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria nchini (Tanzania National Coordinating Mechanism for Global Fund for Aids Tuberculosis and Malaria) hadi Desemba 2014.

Alipata shahada ya Uzamili ya MSc katika Elimu ya Uendelevu kutoka Chuo Kikuu cha London South Bank na shahada ya BA katika Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam. John pia amewahi kuhudhuria mafunzo kadhaa ya kitaaluma katika nchi mbalimbali.

John amefunga ndoa na Mary W.B. Kalage na wamebarikiwa kupata watoto watatu wa kike.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “Tunawapongeza Shirika la HakiElimu Kupata Mkurugenzi Mtendaji Mpya

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.