CCM ITASHINDA TU HATA KWA GOLI LA MKONO!

nauye

CCM imesema kuwa itahakikisha inarudi Ikulu hata “kwa bao la mkono” wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25. Katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye viwanja vya Nyehunge wilayani Sengerema.

“Rangi inayoenda Ikulu ni hii (anaonyesha shati lake la kijani ambayo hutumiwa na chama hicho). Tuna uhakika na ushindi wa Rais. Kwa namna yoyote ile, CCM itarudi Ikulu hata kama ni kwa bao la mkono… bao ni bao tu ili mradi refa hajaona,” Source: MCL

Kwa kauli hizi ni dhahiri namna yeyote itatumika hata kama wakiweka mgombea ambaye hatakubalika kwa kiasi kikubwa.

Lengo ni kuwa na uchaguzi Huru na wa Haki ili sisi kama Watanzania tuliokubali kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa basi tuanze na tuzidi kukua kidemokrasia.

Kila chama kina wagombea wake ambao mpaka sasa wameshafanya mchujo na vingine bado vinaendelea na mchakato wa kumalizia mchujo wa wagombea wao ili wapate yule BORA atakae kubalika kwa Wananchi.

Sasa zinapotokea kauli kama hizi kwa hali halisi ni dhahiri maslahi binafsi yanawekwa mbele na ndio yanayoenda kusababisha matatizo na kupuuzwa kwa maslahi mbalimbali ya Watumishi na wananchi kwa ujumla hususani hali na maslahi ya Walimu.

Nchi yetu inahitaji kubadili mifumo mingi sana ili tuweze kupiga hatua katika nyanja mbalimbali ikiwemo mfumo wa ELIMU. sasa inapofikia viongozi kuingia madarakani bila ya kua na nguvu ya wananchi ni dhahiri utekelezaji wa matakwa ya wananchi utakua mdogo sana.

 

Mungu Ibariki Tanzania

Nini maoni yako kutokana na kauli hiyo ya Nape?

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.