Kama Usivyoweza Kumjua Mke mwema kwa akili zako, Hata Mume Mwema Huwezi Kumjua.

10352937_689585237841195_5304678272195827437_n

Ni kibiblia Kabisa Kuwa Huwezi Kutembea na Mtu Pamoja Kama Hamjapatana.
Nazaidi Sanaa Mungu aliyehai anaheshimu Sana Mapatano ndomaana Hata Israel Walipoenda Yeriko kuipepeleleza Yule kahaba Alipogundua Kuwa Hili Taifa ndilo litakalokuja Kumiliki hapa Kwa Hisani Ya Mungu atawalaye Dunia Alifanya Mapatano nao Kwakuwahifadhi Ndugu zake. Ili Israel watakapokujakuipiga Yeriko Yeye na Nyumba Yake Wapone.


Yoshua 2:1_24
Kadhalika hata Kwa Wale waGibeoni walipatana na Israel Kwakutumia Uongo lkn Mapatano yao Yaliheshimiwa na Mungu na Israel Pia.


Leo nataka niseme kwa Habari Ya Watu Wawili ambao Wamepatana kuwa Marafiki wanaotamani Kuanzisha Safari Itakayowapeleka Katika Kijiji Cha Ndoa.


Kabla Ya Kupatana na Mtu Kwa habari ya Mahusiano Makuu (Ndoa) Omba Sana Muulize Mungu,Ili Mungu ajifunue Kwenu Tena Omba Kwa Gharama huku Ukifunga bila Kuchoka Kwasababu Kwa Macho Yako na kwa akili zako huwez Kujua Yupi ni Sahihi.


Huwez Kumtambua mtu Ubora wake na Uzuri wake wa ndani Kwa akili zako mwenyewe au Kwa mali zake na Pesa zake au Umbo na Sura Yake! Na chochote Ukionacho kwa Macho ya Nyama.


Mithali 31:10
Kama Usivyoweza Kumjua Mke mwema kwa akili zako Hata Mume Mwema Huwezi Kumjua.
Tamani Kuwa Na Mwenzi atakae Kuwa Rafiki Kwako Ukiwa na Mwenzi Rafiki Utakuwa Muwazi Kwake naye Pia atafanya hivyo kwako.


Na zaidi sana Tamani Kuwa na Mtu Unaempenda ambaye Moyo wako Utamfurahia Tena Awe AMEOKOKA KWA WALOKOLE WENZANGU.


Kama Mungu alivyowaambia Wale Mabinti wa Israel Kuwa Waolewe na Wanaume ambao wao Wanapenda Kuwa nao Lakini wawe Waisrael.


Hivyo basi Hata Kwako Iwe Hivyo, Omba Mungu akupe Mwenzi Mtakaependana Kwasababu Katika Upendo Wa Kweli Kuna nguvu ambayo Husaidia Sana Kuyashinda Mambo Yasiyofaa Yenye Kuumiza na Kuliza Kwa Majuto makali.


Wimbo Uliobora 8:6_7
Nguvu ya Upendo Utokao ndani Ya Mtu Hakuna Kitu kinachoweza Kuuzuia ndo maana biblia inasema Upendo unanguvu Kama Mauti.


Mpendwa Mauti hakuna asiyeijua Mauti humnyamazisha Mtu asiweze Kuamka Kamwe!


Sasa Kama Upendo Unanguvu kama Mauti na Wivu wake ni mkali kama Ahera hivi Mkipendana Kwa Huu Upendo Mkubwa ni Kitu gani kiweze Kuunyamazisha Huo Upendo ambao Unanguvu Kama Mauti ambayo hupelekea Kumzika mtu na Tukamsahau kabisa?


Naamini Kabisa Ikiwa Utamuomba Mungu Kwa Dhati ya Moyo na Kwakuvumilia HUTAKUJA KUJUTA KWA MWENZI AMBAYE UTAPEWA NAYE.


Kataa Kuwa na Mtu kwa sababu ya Vitu kwasababu Uwezo wakutafuta Vitu nakupata Tukavimiliki tunao lakini Sirahisi Kupata Mtu atakae Kupenda Kwa Dhati Ya Moyo kwa Akii zako.


Hakuna asiyetamani Kuwa na Mwenzi watakaetembea Pamoja Kwanzia Ujanani hadi Uzeeni Kila Mmoja anatamani sana.


Lakini Kama hutapata Mtu Mwenye Mapendo Tele Kwako HUWEZI KUFIKA SALAMA. Kwasababu Biblia Inasema Upendo Huvumilia Sasa Kama Umependa Vitu na Vitu Vimekwisha Je?


Itakuwaje Hapo?


Haya Mambo Siyo Rahisi Kwa akili zakibinadamu Tunamuhitaji Mungu Kwa Kiasi Kikubwa.


Jitahidi Tuu Usiyachochee Mapenzi Kwa Wakati Usiostahili Ngoja Bwana Akupe Mwenzi Utakae Mfurahia sikuzote za maisha Yenu Mwenzi Ambaye Mungu amekusudia Kukupa Hutashindwa Kuchukuliana nae. 


Acha Kutumia akili zako kwa sababu Mwenzi Wa Maisha Siyo Kiatu Kusema Kisipokutosha Utabadilisha Kingine Kwakukujaribu.


TAMBUA KUWA KUWA NDOA NI AGANO LA MILELE NA UKIKOSEA KATIKA HILO ENEO HATA KAMA UNAMPENDA MUNGU KIASI GANI AMINI USIAMINI LAZIMA UHUSIANO WAKO NA MUNGU UTAHARIBIKA.


KWA SABABU MUNGU ANAHESHIMU SANA NDOA Ndomaana akasema Ndoa na Iheshimiwe na Watu Woote.


JE? Upo tayari Kumuacha/Kuharibu Mahusiano Yako na Mungu kwa ajili ya Mwenzi wako?


Yaaaani Ukose Mbingu eti kwa sababu ya Fulani?!


Hapana MBINGU ZINAUBORA KULIKO HATA WAZAZI WANGU NA CHOCHOTE NINACHOKIJUA NANISICHOKIJUA.


Epuka Adha za kuanza Kukesha na Kuomba Baadae Kumuombea Mtu ambaye Kwa Mateso na Kwa Maumivu makali Baadae Atakusumbua Kataa Roho ya Misukosuko na Migogoro Kwenye Ndoa Mapema! Kataa Kutusumbua Watumishi wa Mungu Baadae Kwaajili Ndoa Ya Mibamiba.


Amua sasa Kutafuta Ndoa itakayokufanya Umkaribie Mungu Kwa Maombi ya Shukrani huku Mkiwafurahia watoto wenu Na watoto wenu wakiyafurahia Maisha yenu.


Mungu akusaidie na Akufanikishe Sana Kijana Mwenzangu.


Nakupenda Sanaa

#HappyRister

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.