Mtoto aliyekosha Ulimwengu kwa ari yake ya Kujituma katika Kusoma!

Mtoto aliyekosha ulimwengu kwa ari yake
Mtoto aliyekosha ulimwengu kwa ari yake

Mtoto aliyepigwa picha akidurusu usiku nje ya mkahawa wa McDonald huko Ufilipino amevutia hisia kali ulimwenguni kote kwa ari yake ya kupata elimu.

Mwanafunzi wa Uuguzi bi Joyce Torrefranca, ndiye aliyeipiga picha hiyo nje ya mkahawa huo wa McDonald ulioko katika mji wa Cebu nchini Ufilipino na akaichapisha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Facebook na ujumbe;

”mtoto huyo amenikumbusha niwekee bidii maishani”

Mtoto aliyekosha ulimwengu kwa ari yake
Mtoto aliyekosha ulimwengu kwa ari yake

Katika picha yake bi Torrefranca mtoto mwenye umri wa miaka 9, Daniel Cabrera amejikunyata kwenye kibao anachokitumia kama meza akifanya mabaki ya kazi aliyopewa shuleni.

Mtoto huyo Cabrera anatumia mwangaza wa bango la kutangaza duka la McDonald kama taa yake akidurusu !

”kwangu mimi kama mwanafunzi ,nilipigwa na mshangao kutokana na ari ya mwanafunzi huyu mdogo aliyekuwa amechutama akikamilisha kazi yake ya shuleni bi Torrefranca aliiambia runinga ya ABS-CBN katika mahojiano.

”kwa hakika ilinipatia changamoto kubwa niendeleee kufanya bidii katika kila jambo linalonikabili”

Muda mchache baada ya bi Torrefranca kuchapisha picha hiyo kwenye Facebook maelfu ya watu waliichapisha pia wakisema kuwa ilikuwa imewavutia sana.

”Ukitaka kitu ama ukitaka kufanikiwa maishani sharti itie bidii katika kila jambo unalokabiliwa nalo,hivyo utapiga umaskini teke” alisema bi Torrefranca.

150711092411_mtoto_aliyekosha_ulimwengu_kwa_ari_yake_624x351_bbc_nocredit

Alipohojiwa kijana huyo Daniel alisema kuwa aligundua babake mzazi alichomwa moto hadi kufa katika ajali mbaya.

Kakake mwengine ni mgonjwa sana alisema Daniel.

Kijana anasema kuwa yeye hulazimika kupiga buku nje ya mkahawa huo wa McDonald kila usiku akimsubiri mamake akamilishe wajibu wake katika mkahawa ulioko karibu.

Afisa wa serikali anayeshughulikia maslahi ya watoto tayari ameitembelea familia ya Daniel kwa nia ya kuwapa msaada wa kujinasua kutoka kwa minyororo ya Umaskini.

Kwa upande wake vyombo vya habari vimekuwa vikimmiminia sifa kochokocho bi Torrefranca kwakuangazia masaibu yanayomkabili kijana daniel.

Chanzo: BBC – Swahili

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.