Nani Abadilike? Kuelekea Elimu Bora yenye Tija

10930067_571818096282561_3761350164147276924_n

Mwalimu anapoingia darasani kwa mara ya kwanza, huwa na furaha sana kwenda kukutana na wanafunzi wapya ambao anatamani kuwafahamu na kujenga urafiki mpya ambao utampelekea yeye ajitume katika kuwafundisha. Kadri siku zinavyosonga ndivyo mwalimu anavyojaribu kuwaelewa wanafunzi wake mmoja baada ya mwingine lengo tu aweze kujua uwezo wao na kuwasaidia katika kile anachokifundisha.

Katika matarajio yasio ya kawaida furaha ya mwalimu hupungua siku hadi siku, kipindi kwa kipindi kadri anavyozidi kuwaelewa wanafunzi wake. Tija ya mwalimu ni kuona wanafunzi wake wote wanafanikiwa kupitia kile anachokifundisha. Atajitahidi kadri awezavyo kufanya wanafunzi wamuelewe; iwe kwa mbinu au njia mbalimbali za kitaalamu anazozifahamu.

Yapo maswali mengi unaweza kujiuliza, kwanini mwalimu anafoka darasani, anatukana, anazira darasa, anakua wakulaumu tuu kila akiingia darasani, anakua mkali; kwanini? Yanaweza kuwepo majibu mengi hapa ila kikubwa ni uchu wa mwalimu kwa mwanafunzi wake afanikiwe; alitamani yale matarajio yake siku ya kwanza kukutana na wanafunzi wake alitamani wawe vile alitamani wawe ili waweze kufanikiwa katika maisha yao kwa kumsikiliza yeye na kushirikiana nae.

Hatimaye anaanza kubadilika furaha yote inayeyuka, hasira zinamtawala; atafundisha kwa kufoka, kukata tama, kutokujali tena, na hatimaye kufundisha kwa mazoea.

Elimu imekua ndio silaha kuu ya kupambana na maisha ya kila siku ya mwanadamu. Ipo misemo kadha wa kadha kuelezea faida ya kua na kupata elimu; mfano, “Elimu ni ufunguo wa maisha”. Hivyo ni dhahiri kuwa bila kuwa na elimu hutaweza kufungua maisha yako. Lakini zipo Elimu za aina tofauti, sasa, ni ipi hasa ambayo ndio ufunguo wa maisha? Ile ya darasani toka kwa mwalimu imekua ndio kwa namna moja ama nyingine ufunguo wa maisha; kwanini? Hutupatia stadi na ujuzi mbalimbali wa kukabiliana na mazingira yetu.

Lakini yapo masuala ya kujiuliza; Je, elimu yetu tunayoipata inatupa nini cha kutosha kukabiliana na changamoto za maisha yetu ya kila siku?

Wakati mwingine utasikia mtu akisema, “yule jamaa amesoma sana lakini muone hana lolote masikini mpaka leo na elimu zake” au “Yule jamaa Yule ata hajasoma ila cheki alivyo tajiri, anapiga kazi kweli kweli, je angesoma?”. Yapo mengi tunaweza kujifunza katika watu hawa wawili ila kikubwa cha kujiuliza ni kwa nini amesoma na bado masikini? Pia tunaweza kujiuliza zaidi, kwani amesomea kitu gani? Je, ndo hicho yeye alikua anataka kukisomea? Kwanini hawezi kutenda kulingana na elimu aliyopata?

Elimu ndio kapata, lakini kwa ajili ya nini? Elimu inahitajika kutoa wahitimu (wananchi) ambao makini wanauwezo wa kujitambua kifikra katika ulimwengu huu kwa kutambua nini afanye, namna gani akabiliane na changamoto na kuzitatua, kuweza kujisimamia, kujiajiri au kutengeneza ajira kwa wengine.

Hakuna tija yeyote itayoleta manufaa kwa kutanua wigo wa udahili wa wanafunzi wengi shuleni na vyuoni bila kuboresha nini hasa wanachoenda kujifunza.  Aidha upimaji wa hicho wanachojifunza nao ubadilike kwa kuzingatia ni nini hasa tunapima? Au tunapima kwa kuwa tunakijua tunachokipima na hatuwezi kupima kile tunachotakiwa kupima?

Lazima tuwe na uzani ulio sawa kwa kuongeza idadi ya wanafunzi na kuboresha kile wanachojifunza na ndio hapo tutakua na matokeo makubwa sasa mazuri na yenye tija.

Uzani ambao utampima mtoto si kwa kile anakifahamu kulingana na alivyosoma bali kuwa na ujuzi utakao mfanya aweze kufikiria ‘nje ya boksi’, aweze kusoma kiufasaha, kufikiria kimantiki, kutatuta na kukabiliana na changamoto za wakati huo na zijazo, kuwa mbunifu, kujibadili kulingana na mazingira, kuwa raia mwema mwenye utii na maamuzi shupavu, kudadavua mambo na mwenye kujiamini.

Aidha wazazi wananafasi kubwa katika maendeleo ya watoto wao kwani kadri mzazi anavyokua karibu na mwanae ndivyo maendeleo yake ya elimu yanakua mazuri zaidi na ndivyo furaha ya mwalimu inapodumu zaidi darasani kwani anamfundisha mtu anaependa kujifunza kile anachokipenda.

Sera za elimu zisizo jenga maana ya matokeo kwa mwanafunzi ni mzigo kwa mwalimu, kwani kila mwalimu anapojaribu kuinyumbulisha na matakwa na mahitaji ya wanafunzi wake anakuta vinapishana hivyo humpelekea kukata tama na kufanya jinsi kilivyo na matokeo yake matokeo kusudiwa huwa makubwa lakini ujuzi anaostahili kuupata mwanafunzi unakua haupo.

Hivyo ni vyema elimu yetu ianze sasa kuzingatia ujuzi kama zao kuu la wahitimu katika ngazi tofauti tofauti za elimu.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.