Wanafunzi wa Shule mbili za Kiriba wasomea Chini ya mti kwa kukosa Vyumba vya Madarasa.

wanafunzi(4)

Wanafunzi wa shule mbili za msingi za Kiriba “A” na kiriba “B” katika   halmashauri ya Musoma vijijini mkoani Mara wanalazimika kusomea chini ya miti  baada ya shule hizo katika kijiji cha kiriba kukabiliwa na upungufu mkubwa wa   vyumba vya madarasa hatua ambayo pia imekuwa ikisababisha kupewa likizo za  mara kwa mara hasa wakati wa msimu wa mvua na hivyo kulazimika kukosa masomo.

Wakizungumza wakati wa Harambee ya kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati na  ujenzi wa miundombinu ya Madarasa,Vyoo na Nyumba za walimu katika shule hizo,baadhi ya walimu wakiwemo walimu wakuu wa shule hizo,wamesema upungufu  huo mkubwa wa vyumba vya madarasa na miundombinu mingine ya shule imekuwa  ikisababisha wanafunzi kusoma katika mazingira magumu hasa wakati wa mvua na   jua kali.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kiriba Bw.Semeni Mkama,akizungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho,amesema uongozi wa kijiji utalazimika sasa  kutunga sheria ndogondogo kwa ajili kusaidia ukusanyaji wa michango kutoka kwa  wananchi ili kuwezesha upatikanaji wa haraka wa fedha za ukarabati na ujenzi  wa miundominu hiyo ya elimu katika shule hizo na hivyo kuwandolea adha mhiyo    kubwa wanayoipata wanafunzi na walimu wao.
Kiasi cha zaidi shilingi milioni 44.8 kinahitajika kwa ajili ya ukarabati na  ujenzi huo wa miondombinu katika shule hizo huku harambea hiyo ikifanikiwa   kukusanya fedha taslimu na vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 8.7.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.