‘Ada elekezi yaja’

 

Stella+Manyanya
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Stella Manyanya

Dodoma. Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, imeanza zoezi la kupanga shule katika makundi ili kuweka viwango vya ada kwa kuzingatia ubora wa huduma na kwamba haitaathiri ubora wa elimu.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya, aliyasema hayo wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema). Mdee alitaka kufahamu iwapo Serikali imebaini kiwango cha gharama kwa kila mwanafunzi kwa shule za bweni na kutwa, iwapo hakitasababisha kuporomoka kwa ubora wa elimu.

Manyanya alisema wizara hiyo imefanya utafiti kuhusu gharama za kila mwanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari.

Baada ya utafiti, wizara yangu ilifanya mazungumzo na baadhi ya taasisi zinazosimamia elimu kwa shule zisizokuwa za Serikali na kukubaliana jinsi ya kufikia viwango vya ada elekezi,” alisema.

Alisema wizara inatarajia ubora wa ada elekezi hautaathiri elimu kwa shule binafsi, kwa sababu itapangwa kulingana na ubora wa miundombinu ya shule.

Katika swali la nyongeza, Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo (Chadema) alitaka kufahamu jinsi Serikali inavyotaka kupanga bei elekezi wakati imeifanya elimu kuwa biashara.

Manyanya alisema siyo mara ya kwanza kwa Serikali kupanga bei elekezi kwa faida ya wananchi na kwamba, imefanyika kwa upande wa huduma ya maji hivyo Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (Ewura) wamefanya.

Mwekezaji awe na fedha ya mitaji na si kutumia fedha zinazotokana na ada ya wanafunzi,”alisema.

Kwa upande wake Mbunge wa Songwe (CCM), Philipo Mulugo alihoji ni lini serikali itakaa na wadau wa elimu baada ya serikali kufanya utafiti na wamiliki nao kufanya utafiti wao?

Akijibu swali hilo, Manyanya alisema gharama za shule zitapangwa kulingana na madaraja na hivyo kutoa bei halisi itakayochochea uwekezaji uliohalisi.

Na Sharon Sauwa, Mwananchi ssauwa@mwananchi.co.tz   

 

 

 

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.