MAMBO 10 KUHUSU HALI YA UKIMWI TANZANIA

 

Okoa Maisha

 Kwa Mujibu wa #Ummy_Mwalimu.

 1. Maambukizi ya VVU kwa upande wa Tanzania Bara ni asilimia 5.3.
 2. Wanawake ndiyo wameathirika zaidi na VVU, (wastani wa asilimia 6.2% kulinganisha na asilimia 3.8 ya wanaume walioathirika).

 3. Katika kila Watanzania 100, watanzania 5 wana maambukizi ya VVU.

 4. Katika kila wanawake 100 Tanzania, wanawake 6 wana VVU

 5. Katika kila wanaume 100 nchini, wanaume 4 wana VVU.

 6. Hali ni mbaya zaidi kwa vijana wenye 15 – 24. Asilimia 10.6 ya kundi hilo wameambukizwa VVU.

 7. Katika kila vijana 100 wenye miaka 15 – 24, vijana 11 wameambukizwa.

 8. Asilimia 50 ya waathirika wanapata dawa za kupunguza makali ya UKIMWI.

 9. Shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu mapambano dhidi ya UKIMWI (UNAIDS), limeweka malengo ya muda wa kati ya tisini tatu (90-90-90) ifikapo mwaka 2030.

(a) 90 – asilimia 90 ya watu wote wanaokisiwa kuwa na VVU wajue hali zao.

(b) 90 – asilimia 90 ya waliobainika kuwa na VVU kuanza kutumia dawa mara moja.

(c) 90 – asilimia 90 ya walioanza dawa waweze kuwa na ufubazo endelevu wa virusi vya UKIMWI mwilini mwao.

 1. #Chukua Tahadhari….

– Pima afya yako ili utambue hali yako na namna ya kujilinda ikiwa umeathirika au hujaathirika.

 • Chukua hatua za kujikinga na maambukizi ya VVU. Epuka vitendo hatarishi vinavyoweza kusababisha kupata maambukizi.
 • Wizara ya Afya, mashirika, taasisi na idara za afya za ndani ya nchi na zile za kimataifa zinafanya kila linalowezekana kuendelea na hatua za kuelimisha na kuwatafutia dawa za bei nafuu, waathirika wote lakini, elimu kwa wale wasioathirika.

 • Kwa hisani ya:
  Ummy Mwalimu, Mb.
  WAMJW
  Dar es salaam
  1 Dec. 2016

  Author: Sir Gunda

  A Friend of Education

  2 thoughts on “MAMBO 10 KUHUSU HALI YA UKIMWI TANZANIA

  1. Asante sana kwa taarifa

   2016-12-06 16:27 GMT+03:00 Walimu na Ualimu :

   > Mwalimu Gunda posted: ” Kwa Mujibu wa #Ummy_Mwalimu. Maambukizi ya VVU > kwa upande wa Tanzania Bara ni asilimia 5.3. Wanawake ndiyo wameathirika > zaidi na VVU, (wastani wa asilimia 6.2% kulinganisha na asilimia 3.8 ya > wanaume walioathirika). Katika kila Watanzania 100″ >

   Liked by 1 person

  Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

  Fill in your details below or click an icon to log in:

  WordPress.com Logo

  You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

  Google photo

  You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

  Twitter picture

  You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

  Facebook photo

  You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

  Connecting to %s

  This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.