Serikali yatangaza Ajira kwa watumishi 71,496 katika sekta mbalimbali

News_2

BAADA ya kusitisha ajira za umma kwa takribani miezi tisa, Serikali imesema katika mwaka huu wa bajeti itaajiri watu 71,496 kwenye sekta mbalimbali ikiwamo elimu, afya na viwanda.

Hata hivyo, licha ya kutaja idadi ya watumishi wapya wanaotarajiwa kuajiriwa katika mwaka huu wa fedha, Serikali haijaweka bayana ni lini hasa ajira hizo zitaanza kutolewa licha ya kuwa imebaki miezi sita mwaka wa bajeti kumalizika.

Akijibu maswali yaliyoulizwa na Nipashe juu ya lini Serikali itaanza kutoa ajira, baada ya kuzisitisha kwa muda, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Florence Temba, alisema Serikali inatoa fursa za ajira kama ilivyoelezwa katika mpango mwaka wa fedha 2016/17.

Katika majibu hayo aliyoyatoa kwa niaba ya Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro, yalibainisha kwamba ajira hizo zitakuwa kwenye sekta ya elimu, afya, kilimo na mifugo. Katika mchanganuo wake, Temba alisema katika sekta ya elimu kutakuwa na ajira 28,957, sekta ya afya 10,870, sekta ya kilimo 1,791, mifugo 1,130,huku maeneo mengine ambayo hayakutajwa, yakitarajiwa kuwa na ajira 28,748.

Wakati Utumishi ikisema hayo, hivi karibuni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mwalimu Ezekiah Oluoch, alilieleza gazeti hili kuwa kwa sasa kuna walimu 30,000 mtaani ambao hawana ajira licha ya kuhitimu masomo yao.

Makamu wa Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Obadia Nyongela, pia aliiambia Nipashe mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa sasa kuna madaktari 1,700 mtaani ambao wana sifa, lakini hawajaajiriwa.

“Kama mwaka huu utaisha bila vibali vya ajira kutoka, maana yake mpaka mwakani kutakuwa na madaktari 2,866 wasio na ajira licha ya kuwapo kwa upungufu wa wataalamu hao,” alisema Dk. Nyongela.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Profesa Ephata Kaaya, alisema wanaendelea kuzalisha wataalamu hao kwa sababu wanajua bado Tanzania ina upungufu wa madaktari.

source: Swahili Times

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

3 thoughts on “Serikali yatangaza Ajira kwa watumishi 71,496 katika sekta mbalimbali

 1. Ngoja tusubr

  Sent from my Huawei Mobile

  Walimu na Ualimu wrote:

  > a:hover { color: red; } a { text-decoration: none; color: #0088cc; } a.primaryactionlink:link, a.primaryactionlink:visited { background-color: #2585B2; color: #fff; } a.primaryactionlink:hover, a.primaryactionlink:active { background-color: #11729E !important; color: #fff !important; } /* @media only screen and (max-device-width: 480px) { .post { min-width: 700px !important; } } */ WordPress.com Mwalimu Gunda posted: ” BAADA ya kusitisha ajira za umma kwa takribani miezi tisa, Serikali imesema katika mwaka huu wa bajeti itaajiri watu 71,496 kwenye sekta mbalimbali ikiwamo elimu, afya na viwanda. Hata hivyo, licha ya kutaja idadi ya watumishi wapya wanaotarajiwa kuaji”

  Like

 2. Kwa faida ya waalimu Na wanafunzi wetu nimeanzisha blog inayohusu masuala ya *ELIMU* blog ni mpya bado sijaanza kuweka materials ila nimesha idesign inaitwa *ELIMIKA* kuiona bonyeza hapa http://konayaelimu.blogspot.com/ usisite kutoa maoni yako tusaidiane kuiboresha kama una maswali unaweza weka hapa then ntapublish ili kusaidia wanafunzi please ni kwaajili ya kuboresha ELIMU 🙏🙏

  Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.