
Na Christian Bwaya
Nilifikiri angenifokea na mimi niliyekwenda kwa shughuli nyingine. Ilikuwa kinyume. Alinihudumia kwa unyenyekevu pengine kwa sababu alijua mimi sio ‘mwalimu’.
Nikajiuliza kwa nini Mwalimu Mkubwa anawakosea heshima walimu wake? Kisa hiki kilinifundisha jambo moja. Walimu ni sehemu ya matatizo ya walimu.
Naam. Walimu ‘waliofanikiwa’ kuachana na chaki ni mwiba kwa walimu wanaofundisha watoto mashuleni. Mwalimu akiachana na ualimu anawageuka wenzake. Anataka kuthibitisha kuwa yeye sasa sio mwalimu tena.
Katika mazingira ambayo taasisi nyingi binafsi zinazofanyia siasa masuala ya elimu kwa kuwanyonya (na wakati mwingine kuwadhalilisha) walimu, ungetegemea walimu kokote walipo wangewasaidia wenzao.
Kwamba kama wewe kitaaluma ni mwalimu na sasa uko kwenye nafasi nyingine (serikalini, NGO, taasisi nyingine) usiwatumie walimu kuwaonesha kuwa wewe sio sasa mwalimu tena. Wasaidie. Wanakutegemea.