HAKUNA KIONGOZI YEYOTE ANAYEKOSA USINGIZI KWA WEWE KUKOSA AJIRA!

Wakati wetu wakati tunasoma tulikuwa tunasoma kwa kushindana sana ili tu upate grade nzuri na upate mkopo chuo kikuu na kimbilio letu kubwa lilikuwa ni kusomea udaktari na ukikosa sana ualimu na tulikuwa na uhakika wa  kupata ajira.

 

DSC08267

Ni miaka takribani kumi imepita tukiwa na mawazo hayo, lakini sasa mambo yamebadilika lakini watu hawataki kukubali kama mambo yamebadilika, bado wana matumaini ya kuwa hali itakuwa sawa kama miaka kumi iliyopita, leo nataka nikwambie kama unafikiri hivo basi UMEPOTEA.

Ni miaka miwili sasa wenye taaluma zile ambazo zilikuwa zikihitajika sana sasa si dili tena, na watu bado wanasubiri matamko mbalimbali ya viongozi labda watawazungumzia hata wao lakini nataka nikwambie hakuna kiongozi yeyote yule anayekosa usingizi kwa kukosa kwako ajira na wala hawana wasiwasi kwani wanasubiri tarehe za mwisho wa mwezi wapokee mishahara yao na maisha yaendelee.

Wengi ambao hatuna ajira tumebaki kulalamika tu mwisho wa siku tunarudi ndani kuangalia TV tu na unajiita msomi asiyeweza hata kuwaza nje ya ajira, nakuhakikishia itafika mahali nyumbani watakuchoka na wewe umebweteka ukisubiri kiongozi fulani akuonee huruma haitakuja kutokea hata siku moja.

Nakushauri kama uko katika kundi hilo;

1. Acha kuchagua kazi kama huna kazi,
Fanya kazi yoyote halali ilimradi unaingiza hata sh.1 itakuwa na kuwa kubwa na hatimaye utaajiri wengine.

2. Fanya kazi za kujitolea.
Omba kazi ujitolee bure kwani saivi hamna mwenye shida na wewe, jitolee kwa dhati utaweza kumshawishi bosi wako akupe kazi.

3. Acha kujifanya msomi na wakati huna impact katika jamii.
Wakati wenzio wako wanachakalika na biashara ndogo ndogo wewe unaleta dharau na kudharau kazi zao, hizo dharau zitakuponza na utaendelea kulalamika mpaka mwisho.

4. Jishughulishe na kitu chochote si lazima kile ulichosomea.
Wakati watu wakiendelea kumaliza vyuo na kulundikana mtaani wakisubiri ajira wewe anza na kitu kidogo kikuze kidogokidogo na mwisho wa siku utashangaa una maendeleo makubwa na hutawaza tena ajira.

Anza sasa hujachelewa, mtaji wa kwanza ni akili yako na nguvu zako, sio lazima uanze na mamilioni ya pesa kuanzisha biashara.

“It doesn’t need money to make money”

Asante.

PIUS J. MULIRIYE@2017

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “HAKUNA KIONGOZI YEYOTE ANAYEKOSA USINGIZI KWA WEWE KUKOSA AJIRA!

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.