Leo ni Kumbukumbu ya Kifo cha Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine – April 12 mwaka 1984!

17883690_1322394584503666_6278304343497397137_n

Leo ni siku ya Kumbukumbu ya Kifo cha Aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine aliyefariki April 12 mwaka 1984 kwa Ajari ya Gari Dakawa – Morogoro,..na katika kuadhimisha siku hii ninakuleta baadhi ya Nukuu bora kabisa kutoka kwake.

“Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu” – Sokoine, 26 Machi 1983

“Wajibu wa kila Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe. Si wajibu wa Taifa kumlisha mtu. Unaweza ukasaidiwa unapopatikana na janga. Lakini kama hakuna janga ni wajibu wa kila mtu aweze kujitosheleza kwa chakula na atoe ziada kwa Taifa” – Sokoine, 4 Oktoba 1983

“Vijana leo wengi wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathini hadi arobaini. Lakini wanaitaka Serikali ndiyo iwaulize mali hiyo wameipata wapi. Hivi kwa nini mzazi asimuulize mwanae, ‘mali hii umeipata wapi?'” – Sokoine, 23 Oktoba 1983

MUNGU ailaze Mahali pema peponi Roho yake ..Amen.

By Pio

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.