ASILIMIA 11 DARASA LA SABA NANYUMBU MBUMBUMBU

Ikiwa maadhimisho ya wiki ya elimu yakiendelea, 11% ya wanafunzi wa darasa la saba huko Nanyumbu Mtwara hawajui kusoma wala kuandika.

18157785_1287194214704038_5619169717073497807_n

Kwa mujibu wa ripoti iliyofanywa na Taasisi ya TWAWEZA kuhusu uwezo wa wanafunzi kujifunza, imeonyesha kuwa asilimia 11 ya wanafunzi wa darasa la saba katika Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara hawajui kusoma wala kuandika.

Nanyumbu ni ya mwisho kati ya Wilaya tisa za Mkoa huo katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba wa mwaka jana huku changamoto kubwa ikiwa ni uhaba wa madarasa, hali inayosababisha wanafunzi kusomea chini ya mti na kwenye vyumba vya madarasa ya nyasi.

Wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Wilayani humo, Ofisa Utafiti Mwandamizi wa TWAWEZA, Richard Temu, alisema utafiti huo ulifanyika katika vijiji 30 vya Wilaya hiyo na Kaya 600 zilihojiwa.

Temu alisema, utafiti huo uliowahusisha wanafunzi wenye umri kati ya miaka saba hadi 16, unaonyesha kuwa asilimia 65 ya wanafunzi wa Wilaya hiyo hawahudhurii darasani huku asilimia 50 ya wanafunzi wa darasa la saba wakiwa hawajui kusoma kiingereza.

Aliongeza kwa kusema kuwa katika utafiti huo, walibaini kuwa asilimia 26 ya walimu hawahudhurii shuleni hali inayoendelea kusababisha ufaulu wa wanafunzi hao kuwa mdogo.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Nanyumbu, Salum Palangyo alisema utafiti huo umewafungua macho na kwamba utatumika katika kufuatilia maendeleo ya elimu.

By Kwanza Tv

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

2 thoughts on “ASILIMIA 11 DARASA LA SABA NANYUMBU MBUMBUMBU

  1. Tatizo ni serikali yetu imekalia siasa badala ya kushughulikia matatizo ya elimu. Shule hazina madarasa wala walimu na wanafunzi wanasomea chini ya mti huku wamekaa chini wao wakiwa wamekaa kwenye viti vya kuzunguka. Hii ndo bora elimu

    Like

  2. Habari mwl. mimi naitwa mwl.IBAHATI V MNGAZIJA nilikua na swali kuhusiana na post zako kuhusu Maana ya fundi mchundo ni nini?

    Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.