Harakati za Marafiki wa Elimu ni nini?

Harakati za Marafiki wa Elimu ni nini?

Ni Harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini.

Recovered_JPEG Digital Camera_13182

Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala
yanayohusu elimu kwa lengo la kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa
programu mbalimbali za maendeleo ya elimu.

Mpaka Kufikia mwaka huu 2018, Harakati hizi zimekuwa na wanachama takribani 41,000 kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania.

Sera na mipango mbalimbali ikiwemo Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na Mpango wa Maendeleo ya Sekondari (MMES) inasisitiza umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake. Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini.

Harakati za Marafiki wa Elimu zinalenga kukuza ushiriki wa wananchi katika michakato mbalimbali ya kuboresha elimu na demokrasia. Madhumuni ya Harakati hizi ni kuwawezesha watanzania kuleta mabadiliko katika elimu.

Harakati za Marafiki wa Elimu pia zitakupa fursa ya kubadilishana mawazo na
uzoefu na watu wengine wanaojali elimu na demokrasia.

Nani anaweza kuwa Rafiki wa Elimu?

Mtu yeyote anaweza kuwa Rafiki wa Elimu! Hakuna masharti. Unaweza kuwa kijana au mzee, mwanamke au mwanaume, mwenye ulemavu au asiye na ulemavu, aliye nje au ndani ya shule.

Licha ya watu binafsi, vilevile tunakaribisha maombi kutoka kwa wanafunzi, wazazi pia na walimu wanashauriwa kujiunga.

Wanawake na wasichana wanakaribishwa kujiunga kwa wingi kwani ushiriki wao una umuhimu wa kipekee katika kusukuma gurudumu la maendeleo ukizingatia kundi hili kihistoria limeachwa pembeni katika ngazi mbalimbali za maamuzi kwa muda mrefu.

Kwa Habari zaidi Bofya hapa PDF-Harakati za marafiki wa Elimu! au Wasiliana nasi kwa SMS au WhatsApp 0674141209.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

2 thoughts on “Harakati za Marafiki wa Elimu ni nini?

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.